Leo nimekula nyoka, mtamu!

Jumong S

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
7,427
Reaction score
10,749
Leo nimetembelea Vetrix kwa bwana mmoja mfuga nyoka, jamaa ana varieties of snakes na wapo wa utalii na waliokomaa huwavuna kwa ajili ya chakula, dawa na uuzaji wa sumu. Basi tuliingia mgahawa wake baada ya utalii, tukaelekea banda la kuchagua kitoweo na tulimchagua laddar snake.

Aisee walikaangwa, na tukaletewa. Walipowekwa kwa sahani huwezi amini kama ni nyoka. Ni watamu kama samaki aina ya kibua na so nutritious. Ni mara ya kwanza kula nyoka, but real watamu.

Ushauri: Watanzania badala ya kuwaua nyoka ni vizuri tuwafuge kwa ajili ya kitoweo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo mfugaji yuko wapi?Je anawakamata vipi na kuwachinja hao nyoka??Manake vitu vingine havitakagi ujuaji
Jamaa anaingia bandani anawakamata kama kuku tu! Issue huwa ni kwenye banda la cobra, ukiona anavyowafukuza na kuwadaka unaweza kutoka nduki!!!

Kuchinja ni easy, anamlaza kwenye kigogo anapiga panga, then anamkatakata mapande, huko jikoni ndo sijui ila kinatoka kitu saaafi kabisa! Mazingira ni masafi Sana...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani ni aina zote za nyoka uliwa au ni baadhi tu? Na kama ni aina zote vipi kwa wale wenye sumu kali sumu yao uondolewaje ili hicho kitoweo kiwe salama?
 
Adui yako mwombee njaa... mi adui yangu namba moja ni nyoka, namba mbili Yanga na namba tatu CCM.
Asprin kuna nyoka ni very friendly hata zaidi ya njiwa. Unaweza kutembea nae hata mfukoni. Sema sura tu, wengine balaa
Adui yako mwombee njaa... mi adui yangu namba moja ni nyoka, namba mbili Yanga na namba tatu CCM.
Asprin kuna nyoka ni very friendly hata zaidi ya njiwa. Unaweza kutembea nae hata mfukoni. Sema sura tu, wengine balaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahyo Muda wa kwenda kuchagua kitoweo hukuona haja ya kupiga picha enhee?
Supu ya nyoka ni too common huku, si kitu cha kushangaza. Mbona Kongo wanakula vyura, nyoka, nyani, minyoo n.k na ni kawaida while Tz tunawashangaa?

Kama hujajaribu Hii makitu tafuta migahawa ya vyakula vya asili vya wachina ulipo, hope u will see it common

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu acha tu nipitwe... hiyo makitu nikionana nayo ni ama zake ama zangu... Mmoja wetu lazima afe au aingie mitini kwa usalama wake...
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…