Leo nimecheka sana

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,735
5,003
Vijana wanataka pepo wanaogopa kufa bhana. Nimefika Baa moja nikaagiza supu na katonic kangu pemben kuna meza kama tayu zimezungukwa na vijana wakila raha na aina mbalimbalu za bia.

Hahahaa haikuchukua muda defender ikapita barabarani. Meza zikakimbiwaaa mabinti waliokuja nao maaskini wamelamba mbili tayari kuamka wanajiuliza

Kumbe ukiona defender imepita ujue kuna walioshuka wanatembea kwa mguu na wamevaa nguo za nyumban ile defender inaenda kuwasubiri mbele

Hhahaaa wakaja jamaa wawili wakauliza chooni walipoenda wakarudi wakawanyaka wale mabinti watatu wakapiga pingu

Pale nikaelewa duniani kila mtu ana mjanja wake. Yani wale mabinti walivyokuwa wakichoka na kuongea sijaamini jamaa wanaweza wakimbia siku ya kiama.

Wameelekea kwenye defender na wamerudi wamemalizia vinywaji vyao na sasa wanaelekea vituo vya polisi kujua wanatokaje. Ushauri tu kama unajua hairuhusiwi kunywa pombe kuanzia saa fulani mpaka saa fulani jikaze tu. Kula starehe huku mnachungulia kama defender imeshapita ama la haipendezi.

Tufuate sheria za nchi tuenjoy kwa amani. Yaani mpaka wanakimbia nabaki nacheka tu shida yote hii ya nini na pesa wanatoa wao.

Kha!

Pongezi kubwa kwa jeshi letu la polisi
 
Yaani SAA nane hii watu bado wanakimbia polisi..
NAKWEDE uko wapi tuonane Ili tupige balimi..
Niko jirani na Victoria price hapa hivyo tunaweza kutana villa au hapa hapa tu mshenga wangu kipenzi
 
Yaani SAA nane hii watu bado wanakimbia polisi..
NAKWEDE uko wapi tuonane Ili tupige balimi..
Niko jirani na Victoria price hapa hivyo tunaweza kutana villa au hapa hapa tu mshenga wangu kipenzi
Wanauzaa biriaan MPWAA???
 
Unadannganya maana saa6+ usiku hata soda hairuhusiwi kuuzwa na wewe wangekubeba, so hii ni CHAI
 
Back
Top Bottom