•√√ Shida hazijawahi kuisha mpaka mwanadam anaingia kabulini, maisha yake ni shida tupu, hivyo hivyo na vyoo haviwezi kutosheleza huko shuleni ndo unakuta matundu 6 ya vyoo then wanafunzi 500 hapo unategemea nini kama siyo UTI sugu, maana usafi tu shida nyingine. Nenda sasa vituo vya mabasi huko ndo kuna kasheshe.
Wakuu kwema? Nina Jambo langu hapa! Nimekuwa nikitembelea maeneo tofauti ya ndani na nje ya nchi. Sasa kwenye suala la choo nimekuwa nikitumia vyenye sink la kuchuchumaa but enzi hizo huko bush ilikuwa Ni vile vya kulenga au unaingia zako pori. Tangu jana usiku nipo hapa Geita na hotel...
Niliwahi kuishi Umasaini (mojawapo ya wilaya za Mkoa wa Arusha) mwaka fulani. Wamasai wana mila ngumu sana. Baadhi ya mila hizo zina hatarisha hata afya zao. Mfano ni hii ya baba wa familia kutokuwa tayari kutumia choo kimoja na wanafamilia hususani mkewe na watoto. Kwao ni kinyume na mila mtoto kumwona baba anakwenda kujisaidia.
Hata serikali ikiwalazimisha kujenga vyoo hawavitumii. Wanaume wanaendelea kwenda kujisaidia vichakani. Masika moja mvua ilinyesha ya kutosha. Maji yakavipitia vinyesi vyao na kwenda kuvirundika kwenye mabwawa. Wakaanza kuchota yale maji na kuyatumia pamoja na kunywa bila kuyachemsha. Kipindupindu kikawapitia na kuwatikisa. Hali haikuwa nzuri kwa kweli