ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 622
- 1,543
Siku kama ya Leo 5/5/1818 huko Trier Ujerumani alizaliwa Karl Marx. Hapa Tanzania 5/5/2014 kilizaliwa Chama Cha Siasa cha mrengo wa kushoto, Chama cha Wazalendo ( Act Wazalendo ).
Marx ni mmoja wa wanamapinduzi wachache Sana duniani ambao walifanya watu kuiona dunia Kwa jicho tofauti kabisa. Andiko lake linaloendelea kusomwa na kusomwa, kuchambuliwa na kuchambuliwa, ni Das Kapital.
ACT Wazalendo ni moja ya Chama cha siasa kinachojitahidi kubadilisha Kabisa namna ya kufanya siasa zetu hapa nchini na Afrika. Kufanya siasa za masuala, siasa za majawabu ya changamoto zetu, siasa za uwajibikaji. Sio kazi rahisi lakini tumedhamiria kuifanya.
Siasa za mrengo wa kushoto ( Ujamaa ) ni siasa za watu. Siasa za kutetea wanyonge. Siasa za ukombozi ( liberation). Siasa za Maendeleo ( developmental). Karl Marx aliweka msingi mkuu na ni wajibu wetu kutafsiri msingi huo kwa mazingira yetu.
Mwanazuoni mmoja alipata kuuliza, " Marx angezaliwa Sumbawanga " ingekuwaje? Angeandika Das Kapital ( The Capital ) ?