Leo nawatukana!

 
andika ww mimi nisome....
 
Nimejikumbusha utunzi wa mashairi! vina na mizani!
 
Tunamtaka Zitto wetu kwenye ulingo wa siasa sasa hivi
 
Hivi jamani Ben ndo imeshindikana kabisa kujua alipo mpaka leo hii?
 
Faru John kapotea, Serikali kashituka,
Na kaburi kufukua, mkuu alivyotaka,
Na vipimo kuchukua, muuaji kumsaka,
Faru john ni mnyama, kwa nini siyo kwa Ben?
 
yule demu wake aliyedai Ben yupo kwa mzee madiba anasemaje?
 
Lakini sio fresh kabisa.MTU kapotea kila MTU amekaa kimya
 
Allen ndugu nakiri, tena pasina kificho,
Hao watu ni hatari, hutoa kucha na macho,
Wafanyapo uguberi, moyoni hawana kicho,
Ela sisi kwa hiyari, ndio tumewapa ficho,
ishirini ishirini, tusirudie makosa.

Sawa,

Ishirini ishirini, tusirudie makosa,
je wafikiri nini, Ben tuvavyomkosa,

alikuwa mshikaji, mawazo akichangia,
yenye ukali wa Chaji, vichwani yaliingia,
wenyewe walijihoji, wapi yalipoanzia,
je wafikiri nini, Ben tuvavyomkosa,

Tuamke, tukamsake Ben

[HASHTAG]#bringbackalivebensaanane[/HASHTAG]
 
Faru John kapotea, Serikali kashituka,
Na kaburi kufukua, mkuu alivyotaka,
Na vipimo kuchukua, muuaji kumsaka,
Faru john ni mnyama, kwa nini siyo kwa Ben?
Kwao Joni ni muhimu,
dola kitu adimu,
wazungu wakija humu,
wazijaza kwenye dumu,
wao wanazifuja!
 

Dotto hivi Zitto Zuberi Kabwe aka Ayatolla Khomeni yupo wapi?
 
Tusi lilipokutoka,
nikajua watashuka,
Roho imenilipuka,
moyo umesikitika,
Hawana imani.

imekuwa mara mbili,
hila zao za tumbili,
wana ndumila kuwili,
baba yao ni jahili,
wamelaaniwa.

idadi wameongeza,
wengine wamewatweza,
wamewageuza chaza,
Kimwili kuwachakaza,
Wanawatesa.

Ben kawa sumaku,
kawavuta na wa huku,
wabebwa mkuku mkuku,
kwenye kiza cha usiku,
Hawarudi.
 
The end of old circle and the beginning of new circle
 
The good shall prevail but evilness will perish forever
 
As it was at the beginning so it shall be at the end
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…