Leo najipongeza, nitakula ulabu mpaka kucheee.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Leo najipongeza, nitakula ulabu mpaka kucheee..

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kashaijabutege, Jan 7, 2011.

 1. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ndugu wana JF

  Niwashirikishe furaha yangu ya kuwa leo nimeweza kulipa karo za wanangu sita. Kwa furaha hii, nimepanga kidogo kilichobaki nikalambe ulabu (ndovu baridiiii) na nibakize sadaka kwa ajili ya kumshukuru Mungu Jumapili. Nawaombea ambao bado hawajatimiza jukumu hili muhimu, Mungu akazibariki kazi zao halali ili nao wakamilishe jukumu hili.

  Nasema :welcome:katika kijiwe changu hapa Kabuteigi tule vitu.
  I wish you an enjoyable week-end while drinking responsibly. I love you all.
   
 2. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Sio Kwamba hicho kidogo ukifungulie Fixed Account ili kila mwezi uongezee, ili mwaka kesho usipate hizi tabu tena zilizokupata mwaka huu???
   
 3. Eng. Smasher

  Eng. Smasher JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 746
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndo tatizo la Wazazi wetu kama hawa hawana PLAN hata hawazi kesho itakuwaje!!
  Anachowaza ni ULABU 2,Vipi hapo home m2 akiugua ghafula ume2nza chochote??!!

   
 4. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kuwashirikisha furaha yangu haina maana kuwa nimepata shida sana kupata karo za wanangu. Nia ni kupeana moyo na wengine ambao wana jukumu kama hili. Naichukulia JF kama familia moja ingawa hatufahamiani au hatukai sehemu moja. That was the only reason. Kwa taarifa, kidogo ninachokisema ni kile nilichowithdraw (leo) kutoka benki na si kwamba akaunti haikubaki na kitu kabisa. I am liquid enough.

  Hata hivyo nakushukuru kwa ushauri ingawa benki haziruhusu kudeposit pesa kila mwezi katika FDR. As a new invention, thanks for your advice.
   
 5. Mbwiga_Plus

  Mbwiga_Plus Senior Member

  #5
  Jan 7, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera sana mkuu wetu..
  Umefanya vizuri sana kuweka kipaumbele kwa hawa kizazi kinachoendelea.
  Nakupa goahead hapo kajinunulie Tusker kadha, bili kwangu.
   
 6. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ahsante. Tuma kwa SMS.
   
 7. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Samahani ndugu kwa kutokukuelewa mimi ulivyosema kilichobaki nilidhani ni KILICHOBAKI... pili hapo kwenye BOLD am sure kuna Accounts kama vile Nyota Children Account angalia hapo chini:- Nyota Childrens Plan : Exim Bank, An Edge Above The Rest

  Nyota


  This Children's account is designed to help parents, to meet financial constraints such as rising cost in education and the basic necessities. To beat the inflation costs, parents need to save money and invest wisely.
  • Monthly saving - Invest/deposit a fixed, small amount* every month in the name of your children. *(Minimum balance - T.Shs. 10,000)
  • Specific term - You can make deposits for a period of 3 / 5 / 7 years.
  • End of term benefits - a healthy accumulated sum with interest.
  • Gifts - These deposits units can be gifted to only child relative.
  • Age Group criteria - Below 18years.
   
 8. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hongera kwa kukamilisha malengo! ila kama ukiweza achana na mipombe haina issue. Utaishia kujuta tu asubuhi baada ya ulabu kuisha kichwani.

  Tena na ninyi wahaya mnapokunywa pombe yote inahamia chini kwenye utu uzima ( i am sure unanielewa)
   
 9. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kaka nashukuru.
   
 10. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ahsante ndugu yangu. Mie pombe inaishia kichwani. Mimi nikinywa nakuwa 'bright' na 'creative'. Kama hunywi, basi jaribu moja leo nitakulipia.
   
 11. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  tuko pamoja... nimelimss Frijilangu.... ni vyombo mpaka majogooo!!!zikiisha nahamia..
   
 12. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #12
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  jamani mwacheni a enjoy maisha kidogo ...
  kaiweka familia yake kwanza (hongear sana)
  na sasa naye afurahie maisha ....
  msileta maisha ya kizungu sana
  ndo maana wengi wako wanakuwa na depression ...
  live like there is no tomorrow...
  ungesema nusu ya hiyo kidogo aiweke bank na nusu aka jipongeze hapo ndo ningekuelewa...
   
 13. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Nimemuuliza kulingana na alivyosema kwenye wording zake, kidogo kilichobaki kumbe shida ilikuwa kwenye definition ya KILICHOBAKI, kumbe kilibaki katika zile alizodraw na sio kwamba chote kilichobaki benki.... now if the former was true basi ingebidi a-save lakini alivyonielewesha kwamba hizo karo zilikuwa ni vijisenti tu na benki bado ana pesa nyingi basi ndo nikamwambia hakuna noma..... i
   
 14. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #14
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  haya kama mmeelewana basi..
  na mie nafurahi....
   
 15. k

  kiparah JF-Expert Member

  #15
  Jan 7, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,176
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
   
 16. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #16
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  hongera mpendwa kwa kutimiza wajibu muhimu kwa familia yako. nimevutiwa na kitu kimoja kwamba baada ya kulipa (naamini umelipa ada za mwaka mzima na sio nusu) ndio unatumia kilichobaki. ingekuwa kinyume chake ningekukemea kwa ukali sana. pia umekumbuka sadaka na kushauri wengine wanywe responsibly. lakini usipuuze waliyoshauri wengine, mwisho wa kulipa za mwaka huu ndio mwanzo wa kuhifadhi utakazolipa mwaka kesho. it is a circle of responsibilities. enjoy your drinks both responsibly and responsively and God bless you mpenzi
   
 17. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #17
  Jan 7, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Naungana na wewe kukupongeza watoto sita si mchecho na huu mwanzo wa mwaka hongera ,uko mitaa gani nami nijongee
   
 18. s.fm

  s.fm JF-Expert Member

  #18
  Jan 7, 2011
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 669
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Halafu ongezea na Grants tot tatu hivi ili ulale vizuri..! Hongera sana
   
 19. LD

  LD JF-Expert Member

  #19
  Jan 7, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ndio mzee jipongeze, na mi nakupongeza, karibu chai.
  eeh na wakati mwingine sio lazima watu wakupongeze kweli,
  mmmmh Raha jipe mwenyewe aisee.
   
 20. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #20
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,362
  Likes Received: 3,195
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye bold, kama wewe ni mkristo anayeujua Ukristo, sadaka haiwezi kuwa kile ambacho ni masalia ya matumizi yako, ni vema ungetenga kabisa sadaka na sio kusema kitakachobaki ndio sadaka.

  Nakupongeza kwa kuweza kulipa karo ya wanao sita, hasa kama ni zile shule ghali(wengine wanatuibia tu), ila kama ni hizi za kata za elfu ishirini ni kawaida tu mkuu huhitaji kupongezwa saaana.
   
Loading...