LWENYI
JF-Expert Member
- Jul 4, 2013
- 1,839
- 2,175
Hakika kumbukumbu zangu leo zimerudi nyuma kama sinema baada ya kubonyeza kitufe cha replay.
nakumbuka nikiwa o-level nilikua nikifanya vizuri kwenye somo la historia, hii ilipelekea mwalimu wa somo hilo kunipenda sana.
kwakua ilikua ni kijijini magazeti hayakuwa yakifika kwa wakati basi mwalimu wetu wa historia alika akienda mjini siku za weekend na kurudi na magazeti na mara tu atapoyamaliza kusoma nilikua wa kwanza kuyapata tena alikua akiniletea mwenyewe darasani.
Taratibu nilikua nayasoma na baadaye nikagundua navutiwa zaidi na makala za siasa na uchumi hii ilipelekea kusoma makala nyingi sana za siasa na katika magazet mbali mbali.
kidogo kidogo nilianza kuvutiwa na siasa lakini sikutaka kuwa mwanasiasa nisiyejua uchumi basi nikaanza kudhamiria kusoma uchumi nikifika kidato cha tano na sita mpaka chuo.
namshukuru Mungu ndoto hiyo imetimia
Muda wote huo sikuacha kufuatilia kwa ukaribu siasa, nilivutiwa sana na uwezo wa wanasiasa vijana sana wa wakati huo kina ZITTO KABWE, na uwezo wao wa kujenga hoja na kusimamia wanayoyaamini hakika nilizidi kuvutiwa na siasa zaidi na zaidi. nilitaka siku moja niwe mmoja wa wale watakao simama na kuchangia maendeleo ya taifa letu bungeni.
Ndoto hii ilikua kubwa na ilimea na kuota mizizi siku hadi siku nilosoma na kumaliza elimu yangu ya chuo na kuanza kufanya shughuli zangu, huku nikiendelea kufuatilia siasa kwa karibu sana
Taratibu nilianza kuielewa na kuipambanua vyema tasnia hii muhimu kwa maendeleo ya taifa lolote lile, nilijipa muda na kuamua kuchukua uzoefu zaidi kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 nilitaka kujionea namna mambo yalivyo hasa kipindi chenyewe cha uchaguzi, nilifuatilia kwa ukaribu sana na kujifunza mengi mno,
Hiki ndicho kipindi nilishuhudia watu ninaowachukulia kama mfano kwangu wakipata misukosuko mingi na haa wengine kupoteza maisha Mwenyezi Mungu Awapokee Marehemu Deo, Mtikila, Mawazo na wengine wengi ambao upepo wa siasa uliwakumba kipindi hicho
hakika hiki ndicho kipindi niichojifunza mengi katika maisha nilijua jinsi ngozi ya mwanasiasa inavyohitaji kuwa ngumu, nilijitafakari sana na kuona bado sijatosha kusonga mbele mapema nilijiona ni mtu ninayehitaji kujiimarisha kila nyanja ya maisha yangu
ni katika wakati huo ndipo nilipojua kwamba siasa haikutaki uwe wewe, siasa inakutaka uwe na ndimi nyingi na usiyekua na msimamo, siasa inakutaka ufuate upepo. hakika ilikua ni ni pigo kwangu nilijiuliza moyoni kwamba je? nipo tayari kutumika kwa maslahi ya watu, je nipo tayari kumsaliti Mungu wangu, je nipo tayari kuacha familia yangu sasa? je nipo duniani kusindikiza majibu yangu mwishoni yakaniambia usiondoke ila jipe muda.
Nikiri kwamba miaka hii miwili tangu nijifanyie tathmin rasmi ya ama kuingia au kusubiri miaka miwili baadae najiona ni mtu mwenye mapenzi na biashara na kulima zaidi, ninajiona na amani zaidi kama nitafanya umachinga wangu bila kuingilia maslahi yao. ninajiona Mungu anaweza kunibariki sana kama nitaamua kuilisha Africa mtazamo wangu na ndoto yangu vinazidi kufifia.
Leo imekua ni siku nyingine yenye tafakuri nzito sana kwenye maisha yangu, wakati naelekea kwenye shughuli zangu nikasema ngoja nipitie kidogo humu kwenye mtandao wetu pendwa niliyokutana nayo ndiyo yanayonisababishia huzuni mpaka wakati huu.
Ni leo ambayo Nimeona tena kwamba watu wanaoweza kusimama wenyewe kwa akili zao wako katika hatari kubwa zaidi popote kwenye uso wa dunia, leo hii Mh. Tundu Antipass Lissu anapigana vita ya pili vita ngumu kabisa vita ya kupigania uhai wake, kangu ni faraja kwakua hakufa wakati waliokusudia naamini Mungu anahesabu dua zetu yakuwa tu wangapi tunamuhitaji shujaa huyu wa sheria hapa Tanzania, na kwakua Mungu hakawii idadi ya tunaomuombea kheri itakua imeshinda mapema na asubuhi.
leo si jamiiforum pekee mpaka huko facebook na mitandao mingine mingi ya kijamii wanamlilia lissu wanalilia Uhai wake Mungu aunusuru. na mimi nasema Pigana kamanda haujawahi kukubali kushindwa pigana sana wakati huu tunaamini utaishinda vita hii na uhai wako utadumu
Watanzania wanakuombea sana Leo ni faraja kubwa kwako kuona kabla ya kufa jinsi watu wanavyokupenda na kukuombea ulizaliwa shujaa, na umeishi kishujaa muda wote hata hili nalo utalishinda
KUTOKA 14:14 "Bwana atawapigania ninyi nanyi Mtanyamaza kimya"
MUNGU IBARIKI TANZANIA. amina.