Shamra shamra za kampeni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinaendelea kushika kasi!
Leo magari yenye chata la mtia nia kupitia Jimbo la Arusha Mjini, Paul Christian Makonda yameonekana yakizunguka mitaa mbalimbali ya jiji la Arusha yakitoa hamasa na ishara ya uzinduzi mkubwa wa kampeni.
Soma pia:
Paul Makonda ateuliwa kugombea ubunge jimbo la Arusha Mjini
View attachment 3468177
Paul Christian Makonda ni jina lililosubiriwa kwa hamu na wananchi wengi kutokana na msimamo wake thabiti na upekee wake wa kusimama na watu. Ni kiongozi aliyekuwa kivutio, sasa akiingia rasmi kwenye ulingo wa ubunge Arusha Mjini.
Uzinduzi rasmi wa kampeni unatarajiwa kufanyika tarehe 12 Septemba 2025 katika Viwanja vya Soweto, Arusha, huku mgeni rasmi akiwa Mgombea mwenza wa Urais, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi.
Hizi ndizo shamrashamra kuelekea siku ya kihistoria kwa Arusha!