GE2025 Leo Magari yenye chata za Makonda na kombati ya kijeshi yameenea jijini Arusha kuelekea uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Shamra shamra za kampeni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinaendelea kushika kasi!

Leo magari yenye chata la mtia nia kupitia Jimbo la Arusha Mjini, Paul Christian Makonda yameonekana yakizunguka mitaa mbalimbali ya jiji la Arusha yakitoa hamasa na ishara ya uzinduzi mkubwa wa kampeni.

Soma pia: Paul Makonda ateuliwa kugombea ubunge jimbo la Arusha Mjini

Your browser is not able to display this video.


Paul Christian Makonda ni jina lililosubiriwa kwa hamu na wananchi wengi kutokana na msimamo wake thabiti na upekee wake wa kusimama na watu. Ni kiongozi aliyekuwa kivutio, sasa akiingia rasmi kwenye ulingo wa ubunge Arusha Mjini.

Uzinduzi rasmi wa kampeni unatarajiwa kufanyika tarehe 12 Septemba 2025 katika Viwanja vya Soweto, Arusha, huku mgeni rasmi akiwa Mgombea mwenza wa Urais, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi.

Hizi ndizo shamrashamra kuelekea siku ya kihistoria kwa Arusha!
 
Bashite huyu huyu aliyekuwa anaongoza Magenge ya kuua watu leo ndio anapambwa hivi?..ila uzuri JINAI huwa haiozi
 
Bashite huyu huyu aliyekuwa anaongoza Magenge ya kuua watu leo ndio anapambwa hivi?..ila uzuri JINAI huwa haiozi
Tafuta ela achana na lugha za jinai haiozi. Wakwere wanasema "If you can't beat your enemies, join them". Waweza kujikuta una miaka 70 unasubiri jinai isiyooza huku watu wanakula maisha. Watanzania tubadili mindset, wenzetu wameshaona maisha yalivyo mafupi na mambo yamebadilika. Wengi wetu wamekalia kuombea mabaya yawakute waliojiongeza. Tunajichelewesha.
 
Lakini huyo bashite wako si ndiye mwenye tuhuma lukuki dhidi ya mauaji ya watu. Au una maanisha na hili pia watu walipotezee?
 
Lakini huyo bashite wako si ndiye mwenye tuhuma lukuki dhidi ya mauaji ya watu. Au una maanisha na hili pia watu walipotezee?
Mkuu kwa wiki 3 mfululizo kupitia Polepole JK na Rostam wametuhumiwa mangapi!?, umeona wakikonda?, point yangu sio watu wapotezee, ila nikipata nafasi nawashauri watu wapambanie matumbo yao, kwa watanzania wa leo hakuna wa kuingia Front kufanya lolote, kuendekeza lugha za jinai haiozi ni kusubiri embe chini ya mnazi. Lazimisha, force connection, kuwa hata CHAWA upate maisha mazuri. Leo hii baba Levo na Mwijaku wana maisha mazuri, wakati ma lecturer wa UDSM bado wanaishi kutegemea kuuza maziwa kwa ng'ombe watano. Mambo yamebadilika, tubadilike pia. Hawa watanzania wa leo sio wa kuwategemea kwenye mabadiliko ya kweli nchini. Ukituliza kichwa utanielewa.
 
Watu kama nyie mko wengi,na ndo mnaturudisha nyuma na harakati zetu.Hata diploma huna,unamdharau Prof??Wahed kabisa wewe
 
Wapumbavu kama nyie mko wengi,na ndo mnaturudisha nyuma na harakati zetu.Hata diploma huna,unamdharau Prof??Wahed kabisa wewe
Diploma sina unanijua!?😅., shida hamtaki kuusikia ukweli. Basi endelea kusubiri Makonda kushtakiwa ICC😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…