Leo katika pitapita zangu jijini Tel-Aviv

Leo katika pitapita zangu jijini Tel-Aviv

Forfofo

Senior Member
Joined
Aug 22, 2024
Posts
161
Reaction score
359
Nawasalumia As-salamu Alaykum, tumsifu Yesu kristu. Habari zenu kwa lugha ya Nyumbani.

Dunia inatuajibisha tunajikuta tunakuwepo mahali ambapo hatupendi kuwa,tupo si kwamaamuzi yetu.

Leo Nimejihurumia. Nikanyong'onyea! Nikawa mnyonge sana!

Kila kipembe ni mzegamzega. Ni uchuuzi tu wa maji. Si Holon, si Petah Tiqwa, si Rishon le Ziyyon, si Bat Yam.

Picha ni ile ile. Ukosefu wa maji! Uhaba wa maji! Mgao wa maji! Hivi sasa huku KUNAWA kwa maji ni hekaya za Abunuwasi jijini Tel Aviv.

Nikaingia benki moja, dumu la maji lililokuwa mlangoni wiki sasa lipo bila maji wala, Hali ni ngumu kiasi hicho.

Tuombeane tu
 
downloadfile-37.jpg

Pole mkuu
 
Back
Top Bottom