Leo katika kumbukumbu

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
636
Reaction score
570
1 Septemba 2024 — Maadhimisho ya miaka 60 ya JWTZ

Rais Mhe Dr. Samia SuluhuHassan, akiwa Amiri Jeshi Mkuu, alihudhuria kilele cha maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Katika hotuba yake, alisisitiza mchango wa JWTZ katika kulinda mipaka ya Tanzania, kusaidia wananchi wakati wa majanga na ajali, pamoja na kulinda amani ndani na nje ya nchi. Pia aliahidi Serikali kuendelea kulijengea uwezo Jeshi hilo kwa zana na vifaa vya kisasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…