Leo January 05, 2017 Ben amefikisha siku 50 tangu simu yake ya mkononi ilipotumika mara ya mwisho

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,281
Anaandika Comred Malisa Godlisten
Leo January 05, 2017 Ben amefikisha siku 50 tangu simu yake ya mkononi ilipotumika mara ya mwisho maeneo ya Mburahati jijini Dar, na zimetimia siku 48 tangu taarifa za kupotea kwake zianze kutajwa.

Benard Focus Rabiu Saanane, Baba wa mtoto mmoja, mwanafunzi wa shahada ya uzamivu (PhD) chuo kikuu cha Maastrich nchini Uholanzi, mwanaharakati wa masuala ya demokrasia na utawala bora, na mtumishi wa CHADEMA Makao makuu hajulikani alipo kwa siku 50 sasa.

Pengine kuna watu wachache wanaojua alipo (waliomshikilia). Au pengine yeye mwenyewe ndiye anayejua alipo. Kuna nadharia nyingi zinazotolewa na watu mbalimbali kuhusu Ben. Wengine wakisema amekufa/kuuawa, wengine wakisema anashikiliwa na vyombo vya usalama kutokana na harakati zake (detention), wengine wakisema amefichwa na chama chake (mkakati wa kisiasa) na wengine wakisema amejificha yeye mwenyewe (kwa sababu anazozijua yeye).

Pengine moja kati ya nadharia hizi inaweza kuwa kweli. Lakini mimi na wewe hatujui ipi ni ya kweli, japo naamini siku moja tutajua ipi ni kweli.

Baada ya siku 50 za kuandika na kutoa taarifa mbalimbali kuhusu Ben, leo January 05, 2017 nasitisha utoaji wa taarifa yoyote kuhusu Ben, hadi itakapohitajika vinginevyo. Hii haimaanishi kuwa juhudi za kumtafuta zimekoma, hasha.! Nitaendelea kumtafuta Ben mimi binafsi na kupitia taasisi ya UTG ambayo inaendelea kufanya hivyo.

Tayari UTG ina mipango mingi inayoitekeleza kumtafuta Ben kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Taasisi za serikali, na baadhi ya mashirika ya kiraia. Kwahiyo juhudi za kumtafuta zinaendelea na kwa sasa ni kubwa zaidi kuliko awali. UTG kama taasisi inaweza kutoa taarifa juu ya juhudi hizo, lakini mimi binafsi sitaandika tena jambo lolote kuhusu Ben, though namuombea usiku na mchana apatikane akiwa hai.

Japo kupatikana kwake akiwa hai au maiti ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu. Naamini Mungu achunguzaye nafsi na mioyo siku moja atatuonesha Ben alipo, whether akiwa hai au akiwa maiti na tutajua yote yaliyotokea hadi kupotea kwake. Tuendelee kumuombea. [HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG].!

Malisa Godlisten
 
Tayari UTG ina mipango mingi inayoitekeleza kumtafuta Ben kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Taasisi za serikali, na baadhi ya mashirika ya kiraia. Kwahiyo juhudi za kumtafuta zinaendelea na kwa sasa ni kubwa zaidi kuliko awali. UTG kama taasisi inaweza kutoa taarifa juu ya juhudi hizo, lakini mimi binafsi sitaandika tena jambo lolote kuhusu Ben, though namuombea usiku na mchana apatikane akiwa hai. Japo kupatikana kwake akiwa hai au maiti ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu. Naamini Mungu achunguzaye nafsi na mioyo siku moja atatuonesha Ben alipo, whether akiwa hai au akiwa maiti na tutajua yote yaliyotokea hadi kupotea kwake. Tuendelee kumuombea. [HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG].!

Hongera sana Comred Malisa Godlisten katika hatua ambayo nimefikia mpaka sasa japokuwa hajafanikiwa bado naamini kwa uwezo wa Mungu Ben-Rabiu Saa nane atakuwa bado yupo salama
 
Dahhhh lets hope amebadilisha number na ameamua kukeep low profile apumzike kidogo.
 
. Indeeed mngefungua case high court waliozikwa kwa sandarusi wafukuliwe mpime Vina Saba kujua ukweli.... it could helped you kwa sasa Muda umekuwa mrefu sana... Baba, mama, mke wana maswali mengi Mungu ni mwema awatie nguvu ni Kipindi kigumu sana...
Pia inakatisha moyo vijana kufanya harakati maana hata Chama chake hakina habari tena Malisa Godlisten ...
 
Baada ya lile gazeti kudai Ben ameonekana mitaani nini kilifuatia? Siyo kwamba taarifa hiyo ndiyo ilibidi iwape break askari, UTG na kila aliyeguswa na hili tatizo?

Labda kama uwe na faida na kupotea kwa Ben ndiyo clue kama ile utaachana nayo.
 
Baada ya lile gazeti kudai Ben ameonekana mitaani nini kilifuatia? Siyo kwamba taarifa hiyo ndiyo ilibidi iwape break askari, UTG na kila aliyeguswa na hili tatizo?

Labda kama uwe na faida na kupotea kwa Ben ndiyo clue kama ile utaachana nayo.
TAARIFA ZA KUONEKANA KWA BEN, NA HEKAYA ZA "KIKARATASI" OFISI ZA MWANAHALISI.

By Malisa GJ,

Mwanahalisi waliweka kidokezo wiki iliyopita kuwa Ben anaonekana mtaani na kwenye vijiwe vya kahawa. Kisha wakamnukuu mjumbe mmoja wa kamati kuu aliyedai kuwa "Ben kajificha ili kujitafutia umaarufu wa kisiasa"

Wakaahidi kwamba toleo la jumatatu ya leo Januaru 02, 2017 wangekuja na taarifa kamili. Kabla ya taarifa hiyo nilihoji mambo machache kuhusu kidokezo hicho cha habari. Nikahoji Ben ameonekana mtaa gani (vijiwe gani vya kahawa)? Lini? Akiwa na nani? Aliyemuona ni nani? Na mjumbe wa kamati kuu aliyesema Ben kajificha ni nani?

Baada ya kuhoji nikapokea maoni tofauti. Baadhi wakisema MwanaHalisi hawajui Ben alipo ila habari hiyo ni "kick" ya kuuza gazeti, na wengine wakasema tusihukumu kabla habari yenyewe kutoka. Tusubiri habari kamili ili tuweze kuhoji tukiwa na taarifa za kutosha.

Mhe.Kubenea alinitafuta kwa simu na tukaongea kwa kirefu kuhusu habari hiyo. Moja ya mambo aliyoniambia Kubenea ni kwamba, Kwanini sikusubiri habari hiyo itoke ndipo nitoe maoni? Nawezaje kutoa maoni kwenye kidokezo cha habari badala ya kusubiri habari kamili.

Hatimaye leo nimesoma habari kamili kwenye gazeti la MwanaHalisi kama ilivyokua ikisubiriwa na wengi. Kama ambavyo wengi tukitegemea gazeti la leo lingejibu maswali yote muhimu niliyouliza wiki jana. Yani Ben ameonekana mtaa gani? Lini? Alionwa na nani? Kwanini aliyemuona hakutoa taarifa polisi? Kwanini Ben ajifiche mtaani na kuiweka familia yake, chama chake na marafiki zake kwenye taharuki? Ben analindwa na intelijensia gani kiasi kwamba anaweza kujificha na Polisi wakashindwa kumpata?

Maswali haya nilitegemea yajibiwe kwa ufasaha kupitia MwanaHalisi ya leo. Lakini MwanaHalisi wameshindwa kujibu hata swali moja kati ya hayo. Yani wameongeza maswali badala ya kujibu maswali. Inaonekana ilikua mbinu ya kuuza gazeti.

MwanaHalisi wanadai taarifa za Ben kuonekana mtaani wamezipata kwenye andiko la mkono (kikaratasi) lilioachwa ofisini kwao mtaa wa Kasaba, Kinondoni na mtu asiyejulikana. Yani kuna mtu asiyejulikana alienda na kikaratasi akakiweka chini ya mlango ofisi za MwanaHalisi.

Kikaratasi hicho kinasomeka "Hamumfahamu Saanane. Sisi tunajua alipo. Wala hatuoni anayetishia maisha yake. Kuna wanaodai kauawa, ni waongo. Kuna kitu wanaandaa, kaa chonjo."

Kwahiyo eti wakatumia kikaratasi hicho kama source ya habari yao. Kikaratasi kilichowekwa na mtu asiyejulikana kinageuka kuwa credible source ya gazeti. Haya ni Maajabu.!

Yani gazeti kubwa lenye heshima kubwa kama MwanaHalisi linaacha kuamini vyanzo vya uhakika linakimbilia kuamini vikaratasi vilivyowekwa na mtu asiyejulikana? Hii ni aibu.

Mhe.Mbowe akiwa mkoani Mbeya alisema Ben ametekwa na hapendi kuongelea sana suala hilo ili watekaji wasije kumdhuru. Inaonekana MwanaHalisi hawakuamini taarifa hiyo ya Mbowe.

Lissu katika mkutano wake na wanahabari akasema inawezekana Ben anashikiliwa na dola kutokana na maandiko yake ya kukosoa serikali hasa elimu ya JPM. Lissu akafika mbali na kueleza kuwa anajua maeneo jijini Dar yanayotumika kutesa wakosoaji wa serikali, na akahofia huenda Ben yumo humo. Inavyoonekana MwanaHalisi pia hawakuamini taarifa za Lissu.

Waziri Mwigulu Nchemba nae akatoa tamko kuhusu Ben akidai ni rafiki yake, akisema anasikitishwa na taarifa za kupotea kwake na kwamba serikali inafanya uchunguzi. Lakini inaonekana MwanaHalisi hawakuziamini pia taarifa hizi.

Jeshi la Polisi makao makuu, kupitia kwa Kamishna Robert Boaz, December 21 mwaka huu lilitoa taarifa kuwa wanafanya uchunguzi juu ya taarifa za kupotea kwa Ben. Sikusikia MwanaHalisi wakisema kitu kuhusu hili.

Lakini cha ajabu wamekuja kuamini kikaratasi kilichowekwa na mtu asiyejukikana. Yani hawakuamini taarifa ya Mbowe, hawakuamini maelezo ya Lissu, hawakuamini taarifa ya jeshi la polisi, hawakuamini taarifa ya Mhe.Mwigulu, lakini wamekuja kuamini kikaratasi kilichowekwa ofisini kwao na mtu asiyejulikana. Ridiculous.!!

Yani taarifa ya kikaratasi zimepewa uzito kuliko taarifa iliyotolewa na Mhe.Mbowe, Mhe.Mwigulu, Jeshi la Polisi na Mhe.Lissu.?? Haya ni Maajabu ya kikaratasi. Kwanini MwanaHalisi waamini zaidi taarifa za kikaratasi kilichoandikwa na watu wasiojulikana kuliko kuamini taarifa rasmi zilizotolewa na vyombo vinavyoshughulikia suala hilo? Hivi kati ya kikaratasi kilichookotwa ofisi na Lissu nani anapaswa kuaminiwa?

Kikaratasi ambacho MwanaHalisi wamekitumia kama source ya habari yao kimeongeza maswali badala ya kujibu maswali ya awali. Kwanini kikaratasi hicho kipelekwe Mwanahalisi tu na sio media house nyingine kama Mwananchi, Majira etc? Kwanini waliokiweka wafiche identity zao? Kama kweli walimuona Ben mtaani kwanini hawakutaja hiyo mitaa?

Kama ofisi za Mwanahalisi zina walinzi usiku na mchana, iweje mtu aje na kikaratasi akiweke chini ya mlango bila kujulikana? Nadhani MwanaHalisi wanahitaji kujieleza vzr kuhusu ukweli wa kikaratasi hicho. Otherwise tutaamini kimeandikwa na watu wa humohumo ndani ili kupenyeza agenda yao kuhusu Ben, kisha kujifanya hawajui kilipotoka.

Nashauri Polisi wachunguze vizuri juu ya ukweli wa kikaratasi hicho. Huenda kuna mengi sana nyuma ya pazia kuhusu hicho kikaratasi.

Kwa ujumla habari ya leo kwenye MwanaHalisi kuhusu Ben imekua na impacts mbili kubwa.

[HASHTAG]#Mosi[/HASHTAG]: imepunguza heshima ya gazeti mbele ya jamii. Wapo watu wameanza kulipuuza gazeti hili baada ya kusoma habari ya leo. Baada ya gazeti kutoa tuhuma kwamba Ben yupo mtaani, wengi walitegemea leo wapate majibu yko wapi, kwahiyo kitendo cha gazeti hilo kushindwa kudhibitisha madai yake, na badala yake wakaja na hekaya za kikaratasi na kujifanya kimetoka kwa watu wasiojulikana. Heshima ya gazeti imepungua.

[HASHTAG]#Pili[/HASHTAG]; habari ya leo imefanya watu wahisi imeandikwa kwa msukumo wa chuki kutokana na tofauti ambazo zimewahi kuwepo kati ya Ben na Kubenea ambaye ni mkurugenzi wa gazeti hilo. Hii ni kwa sababu badala ya gazeti hilo kueleza Ben alipo, limeeleza mambo mengi negative kuhusu Ben ambayo hayakua na ulazima wa kuandikwa leo. Kwa mfano katika aya ya 8 &9 mwandishi ameeleza kuwa Ben aliwahi kumrekodi Dr.Slaa, na kutaka kumpa sumu Zitto Kabwe. Tuhuma hizi za miaka 8 iliyopita hazikua na sababu ya kuandikwa leo.

Kama agenda kuu ni kujua Ben alipo, kwanini wamechomekea mambo yasiyohusiana na agenda hiyo? Mara Ben alitaka kumuwekea sumu Zitto, mara Ben alimrekodi Dr.Slaa, so what?? Hayo yanahusiana nini na kupotea kwa Ben? Hivi watu wakisema habari hii imeandikwa kwa msukumo wa chuki binafsi MwanaHalisi watabisha?

Nashauri menejimenti ya MwanaHalisi ijitafari upya kuhusu siala hili. Tunalijua MwanaHalisi kama gazeti bingwa la habari za uchunguzi, sio MwanaHalisi ya udaku kama ya leo.

Tulitegemea habari ya leo ihitimishe mjadala wa Ben. Tulitegemea kupitia gazeti la leo umma wa watanzania ujue Ben amejificha wapi, kwanini ajifiche? Alionekana lini? Sio kutuletea hekaya za "kikaratasi" kilichoandikwa na watu wasiojulikana. Hii ni aibu.

Gazeti kubwa la uchunguzi lenye heshima kama MwanaHalisi kutegemea source ya vikaratasi kutoka kwa watu wasiojulikana, ni aibu kubwa. By the way kama mnakiri kikaratasi kimewekwa na watu wasiojulikana it means mmeshindwa kujua aliyeandika hicho kikaratasi hicho. Sasa je mtawezaje kumjua aliyemficha Ben, kama mmeshindwa kumjua mwandishi wa kikaratasi? Jitafakarini upya. Mmeanza kupoteza heshima yenu kubwa mliyoijenga kwa jamii kwa muda mrefu. Jisahihisheni. Acheni chuki kwenye mambo yanayohusu uhai wa mtu. Bado mna nafasi ya kujisahihisha, itz not too late yet.!

[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG].!

Malisa Godlisten
 
Damu ya mnyonge haiwezi kupotea bure wote waliohusika ipo siku watailipa .
Nimeona nisikuquote kwenye post ya G Malisa ni ndefu sana itasumbua watumia simu.

Kwahiyo kuna kikaratasi kimeandikwa, Malisa G. anaamua kucrush kikaratasi na polisi wanaamua kucrush kikaratasi kisha kila mtu anaamua kucrush kiratasi. Vipi kama ni kweli walioandika wanajua alipo Ben? Kwanini gazeti linalodai liliachiwa kikaratasi lisiisaidie polisi.

Kesi zote za mauaji (especially serial killers na assassins) hua wanakua na hamu ya kuwa credited na walichokifanya, kwa makala nyingi za matukio haya nilizosoma (Mfano Dennis Rader aka BTK) naamini mhusika anaweza kabisa akawa ameandika hiko kikaratasi. Kisipuuzwe na aliyeleta taarifa asipuuzwe.
Katika kesi za abduction taarifa yoyote ni ya kupewa uzito mpaka pale askari wakijiridhisha kua hii taarifa ni fyongo.
 
Mhh huyu sio rahisi kuwa yupo hai. Ni wazi yamemkuta ya mabwepande ila yeye hakuinekana .....haiwezi kufichwa hivyo itavuja tu siri...bora watu wasome misa tu...lakini tamaa hakuna...walokua wakimtafuta wamempata na kummaliza ..kwa nini tunajipa tamaa atakuja
 
Tofauti na mwezi November mwishoni,na mwezi wa December 2016,ajenda hii ilishika kasi katika social networks!
Mbona sasa kimya?
Tofauti miezi ya Nyuma,Katibu wa UTG Ndugu Malisa,amesema kwa sasa ananyamaza kuhusu maswala ya Ben,Yericko amesema yeye ataposti mapenzi,uchumi na michezo ila siasa HAPANA!
Kwanini?
Ben "amejirudisha" au ajenda imekosa mvuto?
 
Nimeona nisikuquote kwenye post ya G Malisa ni ndefu sana itasumbua watumia simu.

Kwahiyo kuna kikaratasi kimeandikwa, Malisa G. anaamua kucrush kikaratasi na polisi wanaamua kucrush kikaratasi kisha kila mtu anaamua kucrush kiratasi. Vipi kama ni kweli walioandika wanajua alipo Ben? Kwanini gazeti linalodai liliachiwa kikaratasi lisiisaidie polisi.

Kesi zote za mauaji (especially serial killers na assassins) hua wanakua na hamu ya kuwa credited na walichokifanya, kwa makala nyingi za matukio haya nilizosoma (Mfano Dennis Rader aka BTK) naamini mhusika anaweza kabisa akawa ameandika hiko kikaratasi. Kisipuuzwe na aliyeleta taarifa asipuuzwe.
Katika kesi za abduction taarifa yoyote ni ya kupewa uzito mpaka pale askari wakijiridhisha kua hii taarifa ni fyongo.
Kama kuna watu wamefanya dhambi hii, ipo siku watailipa. Ama wakiwa hai au wakiwa wamelala mauti, lazima watailipa. Mungu huwa haachi damu ya mnyonge ipotee bure.


Tofauti na mwezi November mwishoni,na mwezi wa December 2016,ajenda hii ilishika kasi katika social networks!
Mbona sasa kimya?
Tofauti miezi ya Nyuma,Katibu wa UTG Ndugu Malisa,amesema kwa sasa ananyamaza kuhusu maswala ya Ben,Yericko amesema yeye ataposti mapenzi,uchumi na michezo ila siasa HAPANA!
Kwanini?
Ben "amejirudisha" au ajenda imekosa mvuto?
Agenda nadhani imekosa mvuto mkuu
We unaonaje?
 
Mimi naamini Ben yupo Hai, tena naamini hata hapa jukwaani yupo ila akitumia ID nyingine. Siamini kutekwa wala kushikiliwa kwake. Ben Rudi bhana tuendelee kusongesha maisha
 
Kama kuna watu wamefanya dhambi hii, ipo siku watailipa. Ama wakiwa hai au wakiwa wamelala mauti, lazima watailipa. Mungu huwa haachi damu ya mnyonge ipotee bure.
Kuna vitu vingine waTanzania hatushughuliki navyo tunampa mzigo Mungu.

Mafisadi: Mungu atawalipa.
Wabakaji: Mungu atawalipa.
Madikteta: Mungu atawalipa.
Swala la Ben: Mungu haachi damu ya mnyonge.

Tukiacha hii tabia na kushughulika na maswala yetu ipasavyo tunaweza kupata matokeo chanya haraka kuliko kusubiri Mungu ashughulikie wakati ana mizigo mingine.
 
nikifikiria kuhusu ben machozi yananitoka.. kama kuna wahusika sirikalini utawala upate laana nzito
 
Back
Top Bottom