lakin
Mtambuzi kuna sababu ambazo tunaweza kusema zinachangia. ila kabla sijaendelea naomba ninukuu moja ya misemo maarufu sna LIFE STARTS AT 40.
haya tuendelee,
wanaume wengi sana katika kipindi cha kuoana hadi mnamaliza kuzaa huwa anakuwa na hamu ya mwenzie kweli na mara nyingi sana ukaribu huwepo na hata kama anakidumu but family issues kwao bado huwa kubwa sababu kubwa ni ipi??
kwa mtazamao wangu huona sababu ni:-
a) ndio wakati ambao wao kama waanzilish wa familia wanakuwa bize na mambo ya uzazi na ulezi wa watoto wadogo
b)ndio wakati ambao wanaume hupenda zaid kushirikiana na mkewe kwaajili ya maendeleo ya familia hasa mambo ya ujenzi nk hivyo hujikuta akilazimika kuwa karibu na mkewe.
c) ndio wakati ambao mume humuona mkewe kama mrembo na mzuri zaid kwani mwanamke anakuwa bado hajazeeka kiumbo, ngozi, nywele nk
d)wanakuwa wanashare most of their interest like wanapanga matumizi pamoja, watatoka kwenda site pamoja, kununua mapambo ya nyumba pamoja na hata kuanzisha miradi ya maendeleo pamoja.
e) ndio wakati ambao wanakuwa wanajikuta wanapata nafasi za kusimamia ndoa za marafiki zao hivyo most of the times hujikuta wakikumbushiana walikotoka na hata kusukumwa kurekebisha ndoa zao.
baada ya miaka 10 kwenye ndoa hapo ndipo yale niliyonukuu mwanzoni hujitokeza, kwani unakuta sasa maisha yameshawakolea.
baba akiangalia maisha yamemkubali, watoto wanasoma na namna ya kupata ada zao anajua, wamesha zeeka mialiko ya kusimamia ndoa sasa haipo tena ama hawaitaki tena, mwanamke ameshaanza kupata makunyanzi kwani ngozi huanza kuvutika, mwili nao kama ni mbaya huanza maradhi mara mgongo, mara kiuno, mara miguu etc, urembo wa mwanamke huanza kupungua, aina za nguo anazovaa huanza kubadilika etc.
hapa sasa baba unakuta mahitaj yake ya vitu vzr yapo juu zaid kwani kama kawaida wanaume hudanganywa na macho yao, ndipo ishu za nyumba ndogo huanza na kadhia kama hizo.
nini kifanyike??
mwanamke mwenzangu uliyeko ndoani usilemae, fanya kazi, maintain your looks kwa mazoez na aina za vyakula usikubali kuwa mzee kimwonekano. zeeka kiumri ila kimwonekano uwe kijana.jaribu na jitahd sana umvutie mumeo kwa mwonekano ili akuone mrembo kila iitwapo leo.ukiweza kuyahadaa macho ya mumeo huko nje hataona sababu ya kwenda. penda mazingira ya nyumba yako na kila baada ya muda buni kitu kipya mabacho utamshirikisha mumeo hasa kifedha na kiushauri kusudi upate muda wa kuwa nae mara kwa mara lol!
huwaga namsifu saa shoga yangu
cacico yeye kama anaona hali inataka kuleta mushkheri utamsikia hubby naona tupake nyumba yetu rangi nyingine. halafu nimeskia kuna rangi nzuri kweli imetoka ukuta hautapata fungus wala kuloana inauzwa kias kadhaa hapo sasa mumewe huweka mikono kichwan ilasasa bi mkubwa ndo kaamua inabidi tu ajikute anaingia kwenye laini wanaanza tena tripu za madukani kusaka materials. umeona akili ya kaike inavyotumika hapa??