Leo bunge mubashara kisa PM anasoma bajet yake

CHOTABUSARA

Member
Feb 6, 2012
47
48
Nacheka kwa masikitiko sana, yani sasa Bunge litakua linachagua nini vyombo vya habari vionyeshe live na nini visionyeshe, halafu nchi hii inasema kuna uhuru wa vyombo vya habari, au ni "not to that extent" nakumbuka juzi ktk uchaguzi wa bunge la EA lilikua live na leo sababu ya budget ya ofisi ya waziri mkuu lipo live.

Sababu mojawapo ya kuzuia Bunge live ni eti watu hawafanyi kazi wanaangalia bunge, kwa hiyo leo ni ruhusa kutofanyakazi au? Najiuliza wanataka kuficha nini? yani bunge linakua live pale tu wabunge wanapokua hawachangii, hii ni kwanini?

Au kuficha umbumbumbu wa wabunge wa chama tawala? Kuona wabunge wakichangia ni muda muufaka wakujua wawakilishi wetu wanafanya tulichowatuma au la ili tuwahukumu uchaguzi unaofata lakini ndio unaambiwa tutakua hutufanyi kazi tukiwaangalia, si bora kuangali bunge kuliko tamthilia au kujiunga BBC kuangalia habari za ulaya.

TANZANIA MY LOVED COUNTRY, WHERE ARE WE HEADING?
 
Back
Top Bottom