Leo asubuhi Nimeuziwa kikombe cha chai Tshs 1000, bado tunazuiwa kuhoji!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,772
36,664
Wakuu, leo nimesononeshwa mno na hali niliyokutana nayo ndani ya mgahawa mmoja hivi ambapo siku za nyuma (Takribani miezi miwili iliyopita) nilipita hapo kunywa cha kwa Tshs 400. Hii ilikuwa ni kawaida kwa kipindi kirefu kwani nimekuwa nikipita kwenye mgahawa huu mara kwa mara nisafiripo nje ya kituo cha kazi.

Lakini cha kushangaza leo napita sehemu ileile na kuuziwa kikombe kilekile cha chai kwa Tshs 1000. Kuhoji nikaambiwa kuwa sukari wanauziwa bei ya ghali mbaya zaidi kwa shida mno! Huu ni mfano dhahiri wa serikali iliyo madarakani kushindwa kwa kiwango kikubwa kuwatumikia wananchi waliyoiweka madarakani!

Nimejiuliza sana ni nini hasa faida ya kuwa na chombo kinachoongoza nchi na kwakweli nimeshindwa kuziona. Kama jambo dogo la sukari serikali inashindwa, vipi kwa jambo kubwa?

Nimetafakari sana ni watanzania wangapi wanaweza kumudu hili ndani ya nchi yao! Mbaya zaidi ukihoji unakumbana na dola iliyosheheni nguvu, hili ndiyo hasa halikubaliki! Wananchi tuna haki ya kuhoji na kupewa ufumbuzi pale ambapo mambo hayaendi ipasavyo.

Tunaiomba serikali ijikite kushughulikia kero za kila siku za wananchi. Wananchi wanatakiwa kuona fahari wawapo ndani ya nchi yao maana wanaitumikia na kujitolea kwa kila hali kuijenga. Tusiwaache wananchi wakalia ndani ya mioyo yao huku tukiwa na uwezo bado wa kutafuta ufumbuzi wa matatizo tena mapema kabisa.
 
Ni kierere chako tu kwani lazima chai
 
Waluiziwa Sh ngapi sukari kiasi cha kikombe cha chai kupandishwa kwa sh 600?

Uongo mwingine muwe mnawadanganya barvicha wenzenu
 
Kwani kuuziwa chai siku hizi ni siri mpaka unashindwa kutaja jina la mgahawa?

Kwa nini usitaje jina la huo mgahawa ili habari yako ibebe ukweli?

Kwa watu wanaotumia fikra pana watafahamu hii ni habari ya kutunga.

Itendee haki habari yako huku ukielewa kuwa uwongo hutumia lifti kuwafikia walengwa wakati ukweli hutumia ngazi.
 
Wakuu, leo nimesononeshwa mno na hali niliyokutana nayo ndani ya mgahawa mmoja hivi ambapo siku za nyuma (Takribani miezi miwili iliyopita) nilipita hapo kunywa cha kwa Tshs 400. Hii ilikuwa ni kawaida kwa kipindi kirefu kwani nimekuwa nikipita kwenye mgahawa huu mara kwa mara nisafiripo nje ya kituo cha kazi.

Lakini cha kushangaza leo napita sehemu ileile na kuuziwa kikombe kilekile cha chai kwa Tshs 1000. Kuhoji nikaambiwa kuwa sukari wanauziwa bei ya ghali mbaya zaidi kwa shida mno! Huu ni mfano dhahiri wa serikali iliyo madarakani kushindwa kwa kiwango kikubwa kuwatumikia wananchi waliyoiweka madarakani!

Nimejiuliza sana ni nini hasa faida ya kuwa na chombo kinachoongoza nchi na kwakweli nimeshindwa kuziona. Kama jambo dogo la sukari serikali inashindwa, vipi kwa jambo kubwa?

Nimetafakari sana ni watanzania wangapi wanaweza kumudu hili ndani ya nchi yao! Mbaya zaidi ukihoji unakumbana na dola iliyosheheni nguvu, hili ndiyo hasa halikubaliki! Wananchi tuna haki ya kuhoji na kupewa ufumbuzi pale ambapo mambo hayaendi ipasavyo.

Tunaiomba serikali ijikite kushughulikia kero za kila siku za wananchi. Wananchi wanatakiwa kuona fahari wawapo ndani ya nchi yao maana wanaitumikia na kujitolea kwa kila hali kuijenga. Tusiwaache wananchi wakalia ndani ya mioyo yao huku tukiwa na uwezo bado wa kutafuta ufumbuzi wa matatizo tena mapema kabisa.

Muwe mnasoma kabla hamjaingia,ili mjue hiyo ni hotel,café,motel,restaurant au mama ntilie....tafuta hadhi yako.
 
Anza na orodha yako leo chai buku tunataka ikifika mwezi kila ulichonunua tujue bei yake mambo ya kawaida tu
 
sukari kijiko kimoja tu kwenye kikombe inakufanya ulipe nusu ya bei ya kilo ya sukari.

Umejitakia tu, usisingiziea Sukari.!
 
We are missing you JK, tulikudharau tukakutukana kila aina ya tusi, leo hii tunajua umuhimu wako, maisha yamekuwa magumu sana
 
Niujinga kukumbuka watawala waliotutaabisha miaka nendarudi..ukiacha Nyerere alikuwa anajitambua..lkn hawa wengine ni majanga tu...hakuna MTU yoyote kutoka huko CCM atakae ponya hii NCHI....
 
Muwe mnasoma kabla hamjaingia,ili mjue hiyo ni hotel,café,motel,restaurant au mama ntilie....tafuta hadhi yako.
We ch.izi soma uelewe! Kabla ilikuwa inauzwa 400 kwa kikombe na sasa ni 1000 ikimaanisha bei imepanda kwa 600 na hii ni kutokana na ukata wa sukari na bei kuwa juu. Haijalishi itakuwa hotelini au kwa mama ntilie
 
Back
Top Bottom