Wakuu labda nishee uzoefu wangu. Nimetumia smartphone za kila aina kuanzia htc, samsung, iphone, sony, lg n.k. Kusema kweli, hizi smartphone ni kama watu tumekariri majina lakini ni tabu tupu. Tangu nianze kutumia lenovo s890 ni miezi sita sasa ya furaha na amani. Simu hii kwakweli imenifanya nisitamani kabisa smartphone nyingine. Japokuwa battery yake sio kubwa kama iliyotajwa, lakini ndio smartphone pekee ambayo nimesafiri nayo toka moshi hadi dar nikiwa niko full online whatsapp, insta, jf, fb messenger.. huku nimeweka earphones nakula music njia nzima, bado napokea simu za kawaida na msg... kiufupi simu hii kwa heavy usage inakaa na charge 15hrs straight. Kwa simu yenye kioo cha inch 5 nadhani jamaa wamejitahidi sana..