Lengo ni kuingo'a CCM au kuleta maendeleo?

Lengo ni kuingo'a CCM au kuleta maendeleo?

Kuna watu wengi sana hapa wana imani kuwa Wapinzani wa Tanzania wataweza chukua madaraka.
Sijaelewa sijui ni kitu gani kinawapa hiyo imani? Ukiangalia kila upande wamezidiwa wanagongwa.

Dalili nzuri ya kushinda ni serikali za mitaa. Wewe unasema unataka kuing`oa CCM wakati mwenyewe hujielewi.

Wapinzani bado sana hapa kwetu labda kije chama kingine makini. Labda anzisheni TANU na ASP ndio mtaweza kuitia CCM lakini kwa hizi mbwembwe mtagongwa kila sehemu.
 
Maendeleo hayawezi kuja bila kuiondoa CCM ndiyo maana lengo kubwa la kwanza ni kuiondoa CCM madarakani,maendeleo hayaji bila kuwa kitu kimoja ndiyo maana wameungana ili wawe kitu kimoja,maendeleo hayawezi kuja palipo na tofauti ndiyo maana wapinzani wameweza kumaliza tofauti zao na wameungana vinginevyo wasingeweza kuungana.
 
WE MTOA MADA, NAKUJIBU KAMA IFUATAVYO:- ISIPONG'OKA CCM MAENDELEO ITAKUWA NDOTO KATIKA NCHI HII.
Ccm ni PAKA maendeleo ni PANYA, ILI PANYA AISHI LAZIMA PAKA AONDOLEWE TENA KWA NGUVU KAMA ILE YA MISRI, LIBYA n.k
Utawezaje kuitoa madarakani CCM wakati inawafanyia mambo mazuri wananchi? Acha kutisha watu wewe huwezi hata siku moja ukaleta mambo ya Libya au Misri. Na yakitokea mwanao ndio atakuwa wa kwanza kufa.

Acha kutumia hisia vitu vinaenda kwa utaratibu.
 
Maendeleo hayawezi kuja bila kuiondoa CCM ndiyo maana lengo kubwa la kwanza ni kuiondoa CCM madarakani,maendeleo hayaji bila kuwa kitu kimoja ndiyo maana wameungana ili wawe kitu kimoja,maendeleo hayawezi kuja palipo na tofauti ndiyo maana wapinzani wameweza kumaliza tofauti zao na wameungana vinginevyo wasingeweza kuungana.
Mbona sisi tunakula bata tu. au unataka serikali ikuleteee mkate nyumbani kwako? CCM nambari one Afrika nzima. Hata CCM ikigombea Kenya inashinda.
 
Ya lini hiyo? Kabla au baada ya ukawa? Kama ni kabla kwa hujui Wasira alikua mpinzani hasa wa CCM?
Ukawa ndio nini sasa hebu nipe tafsiri yake.
 
Utawezaje kuitoa madarakani CCM wakati inawafanyia mambo mazuri wananchi? Acha kutisha watu wewe huwezi hata siku moja ukaleta mambo ya Libya au Misri. Na yakitokea mwanao ndio atakuwa wa kwanza kufa.

Acha kutumia hisia vitu vinaenda kwa utaratibu.

Inaelekea wewe hauko Tanzania, au ..??
Hivi ndio CCM inavyowafanyia wananchi wake...!!!
Bila ya kutumia nguvu hizi, CCM ingeshaondolewa madarakani zamani kabisa.

mwangosi.jpg
 
Nafikiri huwa tunakosea 1 point,kinachotakiwa kuleta mabadiliko sio MTU,bali ni MFUMO,nashida kubwa kwetu ni mifumo na utekelezaji wa hiyo mifumo,tunaweza kumchagua mtu tunaemuona yuko vizuri sana nakumuweka sehemu husika,ila kama mifumo mibovu ndiyo itayomuongoza still tutabakia palepale au nyuma zaidi.
Muungano huu utakuwa na tija tu endapo utakuwa na malengo na mifumo sahihi suala la migogoro ya jana ama leo sio kigezo cha watu kutoelewana na kusonga mbele. Sina maana ya kubariki ila nakupa uhalisia na ukweli,kuwa kama wamesahau yaliyopita basi wanaweza kusonga mbele nakufika walipokusudia. Wewe kama huamini katika hilo nenda kalale usijiandae halafu utaona yatakayokufika.
Be prepared for future and not rely on yesterday,politics has no yesterday....
 
Wazo la kuiondoa ccm linakuja kwanza maana ni kama unataka kupanda maharage shambani, kusafisha shamba ndio kitu cha kwanza na mavuno ndio maendeleo huku magugu yakifananishwa ccm.
Hivi kama Chenge/EL wanaweza kuungana na Sitta kupitisha katiba ya ccm kuna ubaya gani cdm na cuf kuuanga pia kuikataa!??
Hivi vyama kila kimoja kimeanzishwa kwa maelengo yake na kinafanya mambo yake lakini kwa mara ya kwanza katika historia yao kuna sababu iliyo wazi na vyote vimegongana hapo, nayo ni Katiba Mpya ambayo kwa wenye akili wanajua wazi kuwa ndilo suluhisho la matatizo ya sasa hapa Tanzania. Yakiibuka matatizo mengine huko mbeleni basi watakaokuwepo nao watatengana au kuzidi kuungana kulingana na yatakavyoonekana.

Aliyemwambia wanachama hatuelewan nani alitaka tulale chumba kimoja,nani aliyemwambia tunamaumiv au yy kidonda chake cha nyuma ndyo kinamsumbua hakijapona afuate mambo yao Ukawa atuachie wenyewe tunaehisi hatutendew haki bongo Tz
 
Lengo ni yote mawili..

Unapokata mti japo utakata shina lakini pia inabidi ung'oe na kisiki

Ili usafishe uwanja wako uchafu ambao umeletwa na kichaa na uchafu usirudishe tena huna budi kuutoa chafu nakichaa mwenyewe.
 
Ccm itoke kwanza,hayo mengine mbele ya safari!

Hii akili imewafanya wa Libya hadi leo kutoelewa cha kufanya baada ya kumuondoa Gaddafi. Huwezi kuwa na mpango nusu, lazima mtueleze baada ya kuitoa CCM mtaleta maendeleo gani ili na sisi tujue jinsi ya kuwa hold accountable mkiwa madarakani.
 
Mkuu hili ndilo tatizo kubwa sana tulilonalo. Yaani watu wanataka kutuaminisha tufanye kitu bila hata kujiandaa wakati ushahidi tunao. Baada ya CHADEMA kuwa na wabunge wengi wakawaona wenzao kama choo. Sasa hivi iweje wajikombe kwao?

Mbona sisi tunakula bata tu. au unataka serikali ikuleteee mkate nyumbani kwako? CCM nambari one Afrika nzima. Hata CCM ikigombea Kenya inashinda.

Ni kweli CCM inawenyewe na ndio wanaokula bata.Wengine ni wadandiaji wanaosumbuliwa na njaa kali pamoja na ujinga uliosababishwa na CCM.wakenya siyo wajinga wakukichagua chama kama CCM kama CCM wanabisha wakawaulize KANU.
 
KANU linganisha na TAA haiwezi ikaifikia hata TANU na ASP iweje sasa chama cha wastaarabu CCM. Sasa hivi tunataka kugombea nchi ya South Sudani lazima tuongoze nchi.
 
Back
Top Bottom