Lembeli: Sirudi CCM Ng’o!

Lembeli: Sirudi CCM Ng’o!

chinchilla coat

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2016
Posts
5,107
Reaction score
10,979
pic+lembeli.jpg

Aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Kahama Mjini katika Uchaguzi Mkuu mwaka jana kwa tiketi ya Chadema, James Lembeli amesema hana mpango wa kurudi CCM.

Lembeli alisema licha ya chama hicho kupata Mwenyekiti mpya kimejaa wanafiki, hivyo siyo kazi rahisi kurejea katika chama chake cha zamani.

Akizungumza kwa simu kutoka kijijini kwake, Bulungwa katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama jana, Lembeli alisema anashangazwa na kitendo cha makada wa CCM kumpigia simu wakiwa Dodoma wakidai mbona hakurejea ndani ya chama hicho.

Kabla ya kuhamia Chadema, Lembeli alikuwa Mbunge wa Kahama kwa miaka 10 kupitia chama tawala kuanzia mwaka 2005 hadi 2015 alipoamua kuhama.

Chanzo: Mwananchi
 
Hakuhama alifukuzwa. Hatapokelewa hata skitaka kurudi njia zimekataa.
 
Lembeli yangu ishu ya tokomeza aliyoisimamia ndio alijua kila aina ya wanafiki ccm awezi rudi kwenye unafiki
 
Nampa heko mke wake kweli ameolewa na mwanaume haswa mtu makini anaesimamia kauli zake, kina mpendazoe, mrema na wale ng'ombe wengine waliokatwa mikia ni aibu hata kuwatambulisha kwenye sherehe kuwa ndio mzazi wako, hawakawii kukana hata watoto wao, wana njaa mbaya sana ya kichwani.
 
mkuu weka akiba ya maneno kwenye kusimamia kauli hapo,unawagusa wengi especially kama wewe ni upinzani
 
Akiba ya nini? Mwanaume usiku mnalala anakuambia maneno halafu asubuhi anakuambia fulani kaja kuniomba sasa yale ya usiku tuyaache, haa?! mwanaume anaendesha maisha kwa akili ya jirani?! hovyo tu.
 
Nampa heko mke wake kweli ameolewa na mwanaume haswa mtu makini anaesimamia kauli zake, kina mpendazoe, mrema na wale ng'ombe wengine waliokatwa mikia ni aibu hata kuwatambulisha kwenye sherehe kuwa ndio mzazi wako, hawakawii kukana hata watoto wao, wana njaa mbaya sana ya kichwani.
hahahaha jf
 
Lembeli😱 hata wapiga kura hawana hamu nae,ajiunge na waswezi tu.
 
Back
Top Bottom