Lembeli aunga mkono migomo/maandamano. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lembeli aunga mkono migomo/maandamano.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by samirnasri, Jun 30, 2011.

 1. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mbunge wa kahama james lembeli ameunga mkono migomo na maandamano vinavyoendelea hapa nchini kwa kudai kuwa tanzania sio kisiwa kwa kuwa migomo na maandamano vinatokea pote duniani. Lembeli pia amesema migomo ilikuwepo tangu enzi za mwalimu na kuna watu ambao walichapwa viboko ambao leo hii ni wabunge. Pia kasema inasikitisha wanafunzi wanapanga foleni kwenye benk masaa matatu halafu wakiingia ndani wanaambiwa pesa hazijaingia, katika hali kama hii ni vigumu kwa wanafunzi kukaa kimya hata angekuwa yeye angelalamika. Ameitaka serikali itoe mikopo kwa wakati ili kuepusha migomo. Lembeli pia amewataka wabunge kuacha kujadili mambo ya migomo na maandamano bungeni badala yake waielekeze nini cha kufanya kuliko kunyoosheana vidole. Source: bungeni dodoma.
   
 2. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lembeli ni mmoja wa Wabunge wachache wa CCM wanaosimamia wanachokiamini. Wengi wao waliobakia wameamua kufikiri kwa kutumia Matumbo zaidi. Laiti kama CCM wangekuwa na Wabunge japo watano kama akina Lembeli, leo hii watu wasio na misimamo kama Nape wasingekuwa kwenye nyadhifa za kutunukiwa kama ilivyo sasa.
   
Loading...