Lembeli aunga mkono migomo/maandamano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lembeli aunga mkono migomo/maandamano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by samirnasri, Jun 30, 2011.

 1. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mbunge wa kahama james lembeli ameunga mkono migomo na maandamano vinavyoendelea hapa nchini kwa kudai kuwa tanzania sio kisiwa kwa kuwa migomo na maandamano vinatokea pote duniani. Lembeli pia amesema migomo ilikuwepo tangu enzi za mwalimu na kuna watu ambao walichapwa viboko ambao leo hii ni wabunge.

  Pia kasema inasikitisha wanafunzi wanapanga foleni kwenye benk masaa matatu halafu wakiingia ndani wanaambiwa pesa hazijaingia, katika hali kama hii ni vigumu kwa wanafunzi kukaa kimya hata angekuwa yeye angelalamika.

  Ameitaka serikali itoe mikopo kwa wakati ili kuepusha migomo. Lembeli pia amewataka wabunge kuacha kujadili mambo ya migomo na maandamano bungeni badala yake waielekeze nini cha kufanya kuliko kunyoosheana vidole.

  Source: bungeni dodoma.
   
 2. Shenkalwa

  Shenkalwa JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwani hawa wabunge wa ccm hawaujui ukweli kwamba nchi hii imepoteza muelekeo? wanajua sana tena na wenyewe wanaogopa jinsi nchi hii inavyopelekeshwa chini ya chama chao. Ni aibu. Ninawashangaa baadhi yao kushabikia na kufuata upepo tu hata kama mbunge wao ameongea pumba, pumba, pumba wao wanashangilia. Wanashangilia chochote kiwe pumba, upuuzi na chochote ili mradi kimetamkwa na mwenzao. Inasikitisha sana. Cha kushangaza ukikaa nao huku mitaani wanakuambia ukweli kwamba nchi inaelekea shimoni na wanashangaa mambo yanavyokwenda lakini wakifika mjengoni wanabadilika kabisa. Wenyewe wanaita "Collective responsibility". Kosa kubwa ambalo watanganyika wajifunze ni kwamba kuwaacha wawe wengi mjengoni ni kosa kubwa sana sana. Hawa hawatupeleki kokote. Ni mafundi sana wa kuongea na kushawishi watu wakubaliane na upuuzi wao. Watakushawishi ukubali kwamba nchi imekuwa na maendeleo. Kwao maendeleo ni kuwa na magorofa dsm, kukosa umeme, kukosa maji, kukosa elimu ya uhakika, kukosa huduma na madawa mahospitalini, kulala na njaa, kupanda kwa bei zote hata zile za bidhaa muhimu na za lazima, kuwa na mafisadi wengi kwenye chama na mengi mengineyo. Sasa hivi wanatudanganya baada ya kuongeza kodi ya mafuta ya taa kwamba bei ya mtumiaji wa mwisho haitapanda, hiyo ni kutuona sisi mataahira kama walivyozoea. Wameshindwa kuwakamata wanaochakachua petrol na dizel, ule mkono mrefu wa serikali uko wapi katika hili la uchakachuaji mpaka wanasalimu amri na kuamua kupandisha kodi eti ili kudhibiti uchakachuaji? huu ni upuuzi kwa sababu hii itamuumiza zaidi mtumiaji wa mwisho ambaye ni mwananchi yule mlala hoi kabisa. Halafu wanatuambia bei ya reja reja haitapanda wakati huo huo wanasema kama ikipanda itakuwa ni kidogo tu. Jamani jamani hizi pumba pumba hizi mpaka lini... na nini mwisho wa mambo yote haya????
   
 3. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Hili wanaharakati wanatakiwa kulipinga, inawezekana vipi leo wapandishe mafuta ya taa ilhali bajeti waliyosoma haikusema hayo.Nini maana ya bajeti, leo wanapanga hivi kabla hawajatekeleza wanabadilika.Wapuuzi wale, bora Lembeli umetoa dukuduku, leo utapata ahueni kwani umetoa yanayokukera
   
Loading...