LEMA: Wabunge hatuelewani na viongozi wa Serikali

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
LEMA+PIC.jpg

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema uhusiano usioridhisha kati ya wabunge na viongozi wa Serikali unakwamisha shughuli za maendeleo.
Mbunge huyo ameshauri itafutwe suluhu ili kurejesha mahusiano mazuri baina ya makundi hayo.

Akizungumza leo Machi 10, 2018 katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Arusha, Lema amesema kama hakuna mahusiano mazuri kwa viongozi si rahisi kuwapatia wananchi maendeleo.
"Hili ni suala la utawala bora, leo hii kuna watendaji wa Serikali wanaogopa hata kupiga picha na wabunge, hasa wa upinzani. Jambo hili linapaswa kuondolewa kwani lina athari katika jamii,” amesema Lema.

Amesema wabunge wana nafasi ya kuchochea maendeleo ya wananchi na kuondoa kero zao, kwamba kuna wakati kiongozi wa serikali kutokana na sababu za kiitifaki hawezi kupeleka hoja moja kwa moja kwa viongozi wa juu lakini mbunge anaweza.

"Tufanye kazi pamoja, leo hii tunapitisha bajeti ya mkoa lakini kama hatuna mahusiano mazuri baina yetu, sisi kama viongozi sidhani kama tutafanikiwa,” amesema.
Akijibu hoja hiyo ya Lema Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Idd Kimanta amesema anaamini viongozi wa Serikali wanajua wajibu wao wa kufanya kazi na wadau mbalimbali.

"Utawala bora ni pamoja na kufanyakazi pamoja na nina imani hili linafanyika lakini kama kuna watu wanatengwa hilo ni jambo la watu binafsi,” amesema.

Hata hivyo, Kimanta ametaka viongozi kufanya kazi ya kutatua kero za wananchi na kuachana na mambo ya siasa kwani chaguzi tayari zimepita sasa ni wakati wa kufanyakazi.

Chanzo: Mwananchi
 
Kweli Wakati ni Mwalimu Mzuri

God less Lema amekuwa kifikra, katambua umuhimu wa Mahusiano mazuri na Viongozi wa Serikal wakati ni Huyu Huyu alikuwa akimtukana Zitto alipojitokeza kwenye Ziara ya Rais Kigoma

Lema kaanza kujutia Siasa zake za kishamba za kutukana Viongozi wa Serikal

Wengine waige Misimamo ya Lema
Hongera 'Mandela wa Arusha'
 
Kweli Wakati ni Mwalimu Mzuri

God less Lema amekuwa kifikra, katambua umuhimu wa Mahusiano mazuri na Viongozi wa Serikal wakati ni Huyu Huyu alikuwa akimtukana Zitto alipojitokeza kwenye Ziara ya Rais Kigoma

Lema kaanza kujutia Siasa zake za kishamba za kutukana Viongozi wa Serikal

Wengine Misimamo ya Lema
Hongera 'Mandela wa Arusha'
Wenzako wanakua wewe ndio hukui
 
Hatimaye kabadili gia angani..sasa anabembeleza ushirikiano na serikali..kweli mrisho gambo mwanaume
 
Utashirikiana vipi na mbunge anayemtukana Rais?
Utashirikiana vipi na mbunge asiyemtambua Rais?
Utashirikiana vipi na mbunge asiyeongelea matatizo ya jimbo lake bungeni badala yake anaota ndoto mbaya dhidi ya Rais?
Unashirikiana vipi na mbunge anayeamini Serikali inateka na kuua?
 
Lema kasahau mkuu wa mkoa hata kazi akiwa hajaanza tayari akatukana kuwa tutakudhibiti kama mashoga wanavyodhibitiwa uarabuni.Anategemea kuna mtu atampa ushirikiano? Ninachokiona akili kwa mbali Lema inaanza kumwingia keshajua harudi jimbo la Arusha mjini kaanza kujikomba
 
Kweli Wakati ni Mwalimu Mzuri

God less Lema amekuwa kifikra, katambua umuhimu wa Mahusiano mazuri na Viongozi wa Serikal wakati ni Huyu Huyu alikuwa akimtukana Zitto alipojitokeza kwenye Ziara ya Rais Kigoma

Lema kaanza kujutia Siasa zake za kishamba za kutukana Viongozi wa Serikal

Wengine Misimamo ya Lema
Hongera 'Mandela wa Arusha'
Ameshajua Wananchi wamempuuza na vurugu zake na wamejikita kwenye maendeleo
 
Utashirikiana vipi na mbunge anayemtukana Rais?
Utashirikiana vipi na mbunge asiyemtambua Rais?
Utashirikiana vipi na mbunge asiyeongelea matatizo ya jimbo lake bungeni badala yake anaota ndoto mbaya dhidi ya Rais?
Unashirikiana vipi na mbunge anayeamini Serikali inateka na kuua?
mkuu umemaliza kila kitu
 
Lema kasahau mkuu wa mkoa hata kazi akiwa hajaanza tayari akatukana kuwa tutakudhibiti kama mashoga wanavyodhibitiwa.Anategemea kuna mtu atampa ushirikiano? Ninachokiona akili kwa mbali Lema inaanza kumwingia keshajua harudi jimbo la Arusha mjini kaanza kujikomba
Arudi tu kweye kazi yake ya kujimilikisha magari ya raia wema
 
Utashirikiana vipi na mbunge anayemtukana Rais?
Utashirikiana vipi na mbunge asiyemtambua Rais?
Utashirikiana vipi na mbunge asiyeongelea matatizo ya jimbo lake bungeni badala yake anaota ndoto mbaya dhidi ya Rais?
Unashirikiana vipi na mbunge anayeamini Serikali inateka na kuua?
Hilo la chini kabisa litoe kwenye 'kuamini' wananchi 'wanajua'hivyo
 
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema uhusiano usioridhisha kati ya wabunge na viongozi wa Serikali unakwamisha shughuli za maendeleo.
Mbunge huyo ameshauri itafutwe suluhu ili kurejesha mahusiano mazuri baina ya makundi hayo.

Akizungumza leo Machi 10, 2018 katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Arusha, Lema amesema kama hakuna mahusiano mazuri kwa viongozi si rahisi kuwapatia wananchi maendeleo.
"Hili ni suala la utawala bora, leo hii kuna watendaji wa Serikali wanaogopa hata kupiga picha na wabunge, hasa wa upinzani. Jambo hili linapaswa kuondolewa kwani lina athari katika jamii,” amesema Lema.

Amesema wabunge wana nafasi ya kuchochea maendeleo ya wananchi na kuondoa kero zao, kwamba kuna wakati kiongozi wa serikali kutokana na sababu za kiitifaki hawezi kupeleka hoja moja kwa moja kwa viongozi wa juu lakini mbunge anaweza.

"Tufanye kazi pamoja, leo hii tunapitisha bajeti ya mkoa lakini kama hatuna mahusiano mazuri baina yetu, sisi kama viongozi sidhani kama tutafanikiwa,” amesema.
Akijibu hoja hiyo ya Lema Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Idd Kimanta amesema anaamini viongozi wa Serikali wanajua wajibu wao wa kufanya kazi na wadau mbalimbali.

"Utawala bora ni pamoja na kufanyakazi pamoja na nina imani hili linafanyika lakini kama kuna watu wanatengwa hilo ni jambo la watu binafsi,” amesema.

Hata hivyo, Kimanta ametaka viongozi kufanya kazi ya kutatua kero za wananchi na kuachana na mambo ya siasa kwani chaguzi tayari zimepita sasa ni wakati wa kufanyakazi.

Chanzo: Mwananchi

LEMA KIBURI YAKO NA UJUAJI UMEPATA TIBA, MAGUFULI, WE TULIA TU KWA SASA
 
Naona lumumbas mmepata kichaka! Yaani ni kunya kwa kunya!! Kunyeni kabisa leo sikukuu yenu!!
 
Kweli Wakati ni Mwalimu Mzuri

God less Lema amekuwa kifikra, katambua umuhimu wa Mahusiano mazuri na Viongozi wa Serikal wakati ni Huyu Huyu alikuwa akimtukana Zitto alipojitokeza kwenye Ziara ya Rais Kigoma

Lema kaanza kujutia Siasa zake za kishamba za kutukana Viongozi wa Serikal

Wengine Misimamo ya Lema
Hongera 'Mandela wa Arusha'
Ameanza kunusa njia ya kutokea
 
Back
Top Bottom