Lema: TRA hawatangazi mapato, wanajua kinachoendelea, na serikali itashindwa kulipa hadi mishahara

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,940
19,130
Lema akichangia bajeti ya wizara ya fedha Bungeni amesema kauli za viongozi wa juu zinawatisha wafanyabiahsra kurudi nyuma na wengine kuhama.

Ameongezea TRA hawatangazi mapato sababu wanajua kinachoendelea na hali ikiendelea hivi serikali itashindwa hata kulipa mshahara



Amesema sasa hivi watu wanahamisha fedha sababu ya vitisho na kuna wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wanaojiita ni marais wa wilaya na mikoa na kwenda kutishia wafanyabiashara kuwa watawapa kesi za kutakatisha fedha.

Amependekeza ili kurudi kwenye hali nzuri wafanyabiashara wanatakiwa wawe na confidence na mzunguko wa hela urudi mtaani.

TRA wanaenda kukusanya kodi wakiwa na TAKUKURU na usalama wa taifa
Matumizi ya mipango ya maendeleo mwaka 2016 kati ya bilioni 791 zilizoidhinishwa kutumika katika mafungu yote 9 jumla ya bilioni 323 ni fedha za ndani na hadi kufikia Machi ni Bilioni 18 zimetumika na bilioni 1 ndio fedha za ndani na bilioni 17 ni fedha za nje halafu badohao Wazungu wanawazingua.
 
Alisema ikifika oktoba nguo zinazotubana tutashona modo

Wakati ni mwalimu mzuri , ila tusiache kumuomba Mungu kutusaidia, kwani yeye ni mweza wa yote
 
Wauza nyanya wanalia njaaaaaa!
Washibao wanasema eti ni wapiga dili hao!!!

Sijui tuseme aje?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom