LEMA: Ni wakati gani Rais alipaswa kuchukua hatua?

Godbless J Lema

Arusha MP
Sep 28, 2013
92
2,205
Nimekuwa Mbunge kipindi cha pili sasa, nimeona wabunge wakidhalilishwa kwa njia mbali mbali nje na ndani ya Bunge nimeona wabunge wakina mama wakichaniwa nguo na askari ndani ya Bunge, nimeona Wabunge wakipewa kesi za uzushi na uongo. Nimeona Uchaguzi ukiporwa kwa nguvu na mabavu, nimeona Mawaziri watuhumiwa na wahalifu wa fedha za umma wakilindwa na Bunge na wengine wakishika nafasi mbali mbali za Serikali na Bunge.

Ndio maana ninasema, je Bunge lililokosa heshima na haki, linaweza kutegemea vitendo tofauti na vilivyo tokea kwa Kitwanga? Vyombo vya habari na watu mbali mbali wamesifu kwa njia tofauti uamuzi huu uliochukuliwa na Rais lakini Mimi nauliza maswali yafuatayo: Ni wakati gani Rais alipaswa kuchukua hatua dhidi ya Mh Charles Kitwanga?
  1. Je, ni wakati Kambi Rasmi ya Upinzani ilipotoa Maoni yake kwa Wizara ya Mambo ya Ndani juu ya Kitwanga na Infosys na Jeshi la Polisi au ni wakati au Kitwanga alipoingia akiwa amelewa? Je, wakati gani ulikuwa na masilahi kwa Taifa?
  2. Ni wakati gani Rais alipaswa kuonyesha ujasiri wake, je ni wakati Mh Andrew Chenge anachaguliwa kuwa Kiongozi ndani ya Bunge wakati ana historia ngumu ya matumizi mabaya ya ofisi alipokuwa Mwanasheria Mkuu au ni wakati Kitwanga ameingia akiwa amelewa Bungeni?
Tabia hii ya Kitwanga haikubaliki na haipaswi kuungwa mkono, lakini nitakishangaa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Dr Magufuli amesema ametengeua uteuzi wa Kitwanga kwa kwa sababu ya ulevi ndani ya Bunge. Je, Wananchi wa Misungwi wasubiri maamuzi gani ya Chama juu ya jambo hili ambalo limeidhalilisha Serikali na Chama chao? Ni muhimu sasa Kamati kuu ya CCM ikakutana ili kuwapa faraja na matumaini Wananchi wa Misungwi kuwa Chama chao hakiwezi tena kuvumilia Misungwi ikaongozwa na mlevi, maana yake Kitwanga avuliwe Uanachama na Uchaguzi wa mdogo uitishwe mara moja.

Mwisho, Ujasiri huu wa Magufuli uonekane sasa katika mambo makubwa ya msingi katika Taifa letu kwa mfano, haki na amani ya Siasa za Zanzibar, Mfumo wa Tume huru ya Uchaguzi, Uhuru wa Bunge kuonekana na vile vile kurudisha matumaini ya Wananchi kwa kuwapa Katiba mpya ya maoni yao waliyoyatoa. Vinginevyo, tusipokuwa makini tunaweza kufikiri na kuambiwa kuwa bwawa la kuogelea (Swimming Pool ) ni bahari.

TAHADHARI:
Ninaomba kuufahamisha Umma kuwa sina akaunti yoyote kwenye mitandao ya kijamii kama Twitter, Facebook na kwingineko. Watu wote wanaotumia jina langu wajue wanatenda kosa la jinai.


Godbless Lema (MB)
 
Mbunge wangu usitarajie hatua za haki na hekima toka serikali iliyopo kwenye kujihami na maovu ya kupora haki ya wananchi na kuweka rehani nchi yetu.

Nashauri tukaze buti huku Arusha tufanye kazi kwa bidii na kitaalamu tufanikishe ndoto zetu. Hasa ndoto ya UJASIRI WA KUTHUBUTU na kujituma kwa bidii tukiongozwa na Mwenyezi Mungu tusiondoke nje ya mstari wa haki.

Migufuli anawakingia CCM na maovu yao. Kwa sababu yeye mwenyewe analazimika kulinda uovu wake na waliomweka madarakani
 
My Brother, The duties of a leader in functioning democracy is to serve the will of the people.

We do not have functioning democracy. Our current consititution itself embraces authoritarianism

Hivi mtu aliyejilundikia madaraka yote ya Alpha na Omega, aliyeaminisha taifa kuwa amechukua muda mrefu kufanya vetting ili apate mawaziri bora kabla ya kuwateua na baadae kuishia kuteua walevi na sasa anataka asifiwe kwa kutengua uteuzi unaweza ukamuamini kuwa atafuata haya unayomshauri?


Kwamba yeye suala la Infosy na Lugumi lilionekana sio kosa kubwa linalohatarisha mustakabali wa taifa linalozingatia utawala bora juu ya misingi ya Transparency and Accountability lakini Safari Lager na Konyagi za Waziri husika zikaonekana ndio tishio hasa

Huyu Rais wa Aina hii tukimuambia jipu kuu ni Katiba ya sasa kwa hiyo alitumbue kwa kurejesha rasimu ya wananchi iliyorejesha misingi yote muhimu ya taifa anatuona wachawi

Anataka eti tuamini kuwa misingi ya Urais wake ni zile pushups na kucheza Rhumba jukwaani .

Prof.Wole Soyinka Once Said "The man dies in all who keep silent in the face of Tyranny".
 
Mkuu Lema, inawezekana ni kweli alikuwa amelewa. Lakini imani tuliyonayo baadhi yetu nikuwa, Kitwanga alilewa kwa malengo maalum waliyoyapanga pamoja na chama chake CCM ili aonekane kafukuzwa kwa hoja ya ulevi ili kuua so la LUGUMI KIAINA. Tusitegemee Kitwanga afukuzwe uanachama na hasa ukizingatia ambavyo CCM wanaogopa uchaguzi huru na wa haki. Kurudia uchaguzi kwao itakuwa ni kuchezea bahati.
 
Watanzania ni watu wa kupelekeshwa na matukio.

Binafsi naamini kuna kitu nyuma ya ulevi wa Kitwanga.
 
Noted:

1: Katiba Mpya...✔ ( Ya Warioba )
2: Tume Huru ya Uchaguzi..✔
3: Bunge kuonekana LIVE..✔
4: Amani ya Siasa Znz..✔

Ya Chenge na Kitwanga, I, personally siyapi emphasize sana, ILA HAYO 4, muhimu sana, G. Lema hongera sana.. uko very ACTIVE....✔ watu siku hizi hatuangalii chama, tunaangalia mtu... Hongera sana sana...!!
 
Magu alikosa tu ujasiri wa kumfukuza moja kwa moja kwa tuhuma za Lugumi ila hili la ulevi ndio kidogo likamrahishia/likampa nguvu na sababu ya ziada ya yeye kufanya uamuzi wa kumfuta kazi vinginevyo asingefukuzwa kwa kosa la ulevi tu.
 
Nimekuwa Mbunge kipindi cha pili sasa ,nimeona Wabunge wakidhalilishwa kwa njia mbali mbali nje na ndani ya Bunge nimeona Wabunge wakina mama wakichaniwa nguo na askari ndani ya Bunge, nimeona Wabunge wakipewa kesi za uzushi na uongo. Nimeona Uchaguzi ukiporwa kwa nguvu na mabavu, nimeona Mawaziri watuhumiwa na wahalifu wa fedha za umma wakilindwa na Bunge na wengine wakishika nafasi mbali mbali za Serikali na Bunge.

Ndio maana ninasema, je Bunge lililokosa heshima na haki, linaweza kutegemea vitendo tofauti na vilivyo tokea kwa Kitwanga? Vyombo vya habari na watu mbali mbali wamesifu kwa njia tofauti uamuzi huu uliochukuliwa na Rais lakini Mimi nauliza maswali yafuatayo: Ni wakati gani Rais alipaswa kuchukua hatua dhidi ya Mh Charles Kitwanga?
  1. Je , ni wakati Kambi Rasmi ya Upinzani ilipotoa Maoni yake kwa Wizara ya Mambo ya Ndani juu ya Kitwanga na Infosys na Jeshi la Polisi au ni wakati au Kitwanga alipoingia akiwa amelewa? Je, wakati gani ulikuwa na masilahi kwa Taifa?
  2. Ni wakati gani Rais alipaswa kuonyesha ujasiri wake ,je ni wakati Mh Andrew Chenge anachaguliwa kuwa Kiongozi ndani ya Bunge wakati ana historia ngumu ya matumizi mabaya ya ofisi alipokuwa Mwanasheria Mkuu au ni wakati Kitwanga ameingia akiwa amelewa Bungeni?
Tabia hii ya Kitwanga haikubaliki na haipaswi kuungwa mkono, lakini nitakishangaa Chama cha Mapinduzi (CCM) , Rais Dr Magufuli amesema ametengeua uteuzi wa Kitwanga kwa kwa sababu ya ulevi ndani ya Bunge. Je, Wananchi wa Misungwi wasubiri maamuzi gani ya Chama juu ya jambo hili ambalo limeidhalilisha Serikali na Chama chao? Ni muhimu sasa Kamati kuu ya CCM ikakutana ili kuwapa faraja na matumaini Wananchi wa Misungwi kuwa Chama chao hakiwezi tena kuvumilia Misungwi ikaongozwa na mlevi, maana yake Kitwanga avuliwe Uanachama na Uchaguzi wa mdogo uitishwe mara moja.

Mwisho, Ujasiri huu wa Magufuli huonekane sasa katika mambo makubwa ya msingi katika Taifa letu kwa mfano , haki na amani ya Siasa za Zanzibar , Mfumo wa Tume huru ya Uchaguzi, Uhuru wa Bunge kuonekana na vile vile kurudisha matumaini ya Wananchi kwa kuwapa Katiba mpya ya maoni yao waliyoyatoa. Vinginevyo, tusipokuwa makini tunaweza kufikiri na kuambiwa kuwa bwawa la kuogelea (Swimming Pool ) ni bahari .

TAADHARI: Ninaomba kuufahamisha Umma kuwa sina akaunti yoyote kwenye mitandao ya kijamii kama Twitter, Facebook na kwingineko. Watu wote wanaotumia jina langu wajue wanatenda kosa la jinai.

Godbless Lema (MB)
Mkuu binafsi nimekuelewa pamoja na azimio lako Juu ya Bw. Kitwanga. Ila ukakasi unakuja je ni vipi kuhusu muhumili wa Bunge nimaanisha "mjengoni" ambapo kwenu ninyi ndio kama ofisi kuu, ni ruksa kwa mbunge kuingia akiwa ametumia kilevi? Au je kama sheria na kanuni zipo kimya unahisi kunahaja ya kuwepo sheria ya kuzuia jambo hilo.?
Mwisho umesema huna account yoyote katika mitandao ya kijamii je na humu ni hiki ni nini. Kule Face book napo? Uhoni unawaweka wafuasi wako katika njia panda?
 
Mkuu Lema, inawezekana ni kweli alikuwa amelewa. Lakini imani tuliyonayo baadhi yetu nikuwa, Kitwanga alilewa kwa malengo maalum waliyoyapanga pamoja na chama chake CCM ili aonekane kafukuzwa kwa hoja ya ulevi ili kuua so la LUGUMI KIAINA. Tusitegemee Kitwanga afukuzwe uanachama na hasa ukizingatia ambavyo CCM wanaogopa uchaguzi huru na wa haki. Kurudia uchaguzi kwao itakuwa ni kuchezea bahati.

all process was STAGED, hata mimi naamini hivo
 
Back
Top Bottom