Lema: Nawatakia kila la heri madiwani waliohama na kujiunga na CCM

Lema: Nawatakia kila la heri madiwani waliohama na kujiunga na CCM

Godbless J Lema

Arusha MP
Joined
Sep 28, 2013
Posts
92
Reaction score
2,205
Ninawatakia kila la kheri Madiwani waliojiunga na CCM leo katika nchi yenye mfumo wa siasa za vyama vingi uamuzi kama huu unaweza kuwa sawa kama utashi wa maamuzi haya ungewezwa kujengwa katika maadili na ukweli.

Safari hii ya mageuzi ya kujenga demokrasia ni safari ngumu sana wengi wameamua kuuza haki na utu wao na wengine wataendelea, bila shaka ni dhahiri kuwa Taifa letu linapita katika changamoto nyingi kwa sasa kushambuliwa kwa demokrasia kwa njia yoyote Ile sio hasara ya CHADEMA bali ni hasara ya nchi yetu.

Kwa mtu mwenye akili timamu hata ndani ya CCM huwezi kuruhusu kuuawa kwa demokrasi ya Nchi kwa sababu tu ya faida mfu ya chama chako madhara makubwa kichama hayako kwetu bali zaidi yatakuja kuonekana huko CCM kwani hatuna muda mrefu biashara kama hii italeta shida ndani kubwa ndani yao na chama tawala kinapokosa busara ya kutawala sio faida kwa upinzani bali ni hasara kwa Taifa.

Hata hivyo nafikiri tuko kwenye wakati mzuri sana wa mageuzi ya nchi yetu tunapaswa kujipa muda kidogo, haikuwa kazi rahisi Israel kutoka Misri na na kufika Kanaani lakini walifika.

Nchi hii itafikia kilele muhimu cha haki mara nyingi mambo mengi katika Dunia yana amuliwa na muda, tafadhali msiwaze chuki dhidi yao kwani watu wa hii wanaendelea kuwa msaada wa utafiti kwetu wa fikra ndani ya nchi yetu nakufanya tathimini ya kweli ya safari hii muhimu ambayo sijui tutafika lini lakini lazima kuwepo kwenye lengo bila kuyumba ili uhuru wetu uonekane kesho.

Arusha MSIOGOPE.
 
Amen.
Ukitazama kwa jicho la tatu huu mchezo wa hama hama ni mchezo wa chama cha Kijani wa kujitekenya na kisha kujichekesha mwenyewe.

Kwa mwenye akili yeyote anajua mwisho wa hii abracadabra ni aibu tu.

Ila all in all mapambano lazima yaendelee na Tanzania mpya inakuja.

Mungu ibariki CHADEMA.
Mungu ibariki Tanzania.

Amen.
 
Mh. Lema nina wazo hili, lifanyie kazi:
. Waite wale mawakala wote to give a story of what transpired during casting of ballots! Kila mmoja atoe madhira aliyokutana nayo. Yawe recorded, in voice and paper ; and then published to keep records for future use!
 
Huyo nae
Badala ya wao kujibadilisha na kuongelea maendeleo na nini wanataka kufanyia wananchi kwa mazuri na kujipaisha
Wao fujo tu na kulalamika kwa kulia lia mifandaoni na kwenye majukwaa kuhamasisha fujo.

Lazima atakuwa amelia.. eti haki haki wao kama Chadema wananini haswa.. maana wameshindwa kujibadili na kuvutia viongozi kukaa.. walie tu wamejaa tamaa ya wao kujaza matumbo.. na hawajui uongozi wa upinzani kabisaaa.
 
Ni heshima kwa Mungu kumzomea fisadi Lowasa ------Lema .

Lakini leo wewe Lema ndio mbeba mabegi wa Lowasa ,tukueleweje??

Shambulio la democrasia hutokea tu ambapo mtu akihama chadema kwenda chama kingine?

Vipi wanaotoka vyama vingine kwenda chadema hapo hamna shambulio la democrasia??
 
Solution nzuri. Kila mwakilishi wa mwananchu wa chadema aitishe press conference atangaze either anaunga mkono au anabaki
Full stop
 
''Diwani mmoja amesema; "Hakuna maisha magumu kisiasa kama kuishi kwenye Ukoo wa kambale ambao Baba, Mama na watoto wote wana Ndevu. Agenda hakuna, kila Mtu mropokaji na kulazimishana kufanya siasa za kuhujumu maendeleo kama njia ya kuijenga Chadema badala ya Nchi. Tukiendelea na siasa za namna hii, itafika wakati tutaambiwa tukabomoe Madaraja na kuiba pampu za miradi ya maji? '' kuna tatizo mahali
 
Huyo nae
Badala ya wao kujibadilisha na kuongelea maendeleo na nini wanataka kufanyia wananchi kwa mazuri na kujipaisha
Wao fujo tubna kulalamika kwa kulia lia mifandaoni na kwenye majukwaa kuhamasisha fujo.

Lazima atakiwa amelia.m etibhaki haki wao kama Chadema wananini haswa.. maana wameshindwa kujibadili na kuvutia viongozi kukaa.. walie tu wamejaa tamaa ya wao kujaza matumbo.. na hawajui uongozi wa upinzani kabisaaa.
Andika vizuri acha papara
 
Huyo nae
Badala ya wao kujibadilisha na kuongelea maendeleo na nini wanataka kufanyia wananchi kwa mazuri na kujipaisha
Wao fujo tubna kulalamika kwa kulia lia mifandaoni na kwenye majukwaa kuhamasisha fujo.

Lazima atakiwa amelia.m etibhaki haki wao kama Chadema wananini haswa.. maana wameshindwa kujibadili na kuvutia viongozi kukaa.. walie tu wamejaa tamaa ya wao kujaza matumbo.. na hawajui uongozi wa upinzani kabisaaa.
Soma vizuri ulichoandika hueleweki kabisa umepanic nini???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom