Lema na Nyerere kutikisa mkoa wa Mara

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), anatarajia kuzuru Butiama, mkoani Mara kwa ajili ya kutoa shukrani katika kaburi la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Lema amefikia hatua hiyo baada ya Mahakama ya Rufaa kumrudishia ubunge wake.
Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere, alisema ziara hiyo inatarajiwa kufanyika baada ya msimu wa sikukuu kwisha.
Nyerere alisema Lema atakwenda kutoa shukurani, kwani awali aliponyang’anywa ubunge alikwenda kuomba haki itendeke katika rufaa.
“Tunakwenda na Lema katika kaburi la Baba wa Taifa, amesema anataka kwenda kutoa shukrani baada ya kupata ubunge wake alionyang’anywa na mahakama. Unajua hapo awali alikwenda Butiama katika kaburi na kuomba atendewe haki na kweli haki imetendeka,” alisema Nyerere.
Nyerere pia alisema kuwa baada ya kutoka Butiama watafanya ziara katika Mkoa wote wa Mara yenye lengo la kuhakikisha wanawavua wananchi magamba na kuwavalisha magwanda.
Alisema katika ziara hiyo watatoa elimu na kutangaza sera ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi wa wenyeviti wa serikali za mitaa.
Akizungumzia ziara yake aliyoifanya Kasamwa, Kakolwa, Kyela, Iringa na Tunduma, alisema kuwa ilikuwa na mafanikio makubwa.

Source:Tanzania Daima

My Take:
Godbless Lema na Vicent Nyerere ni kati ya wabunge wa CHADEMA wanaofanya kazi kubwa kuzunguka nchi nzima kuimarisha chama na kueneza elimu ya Uraia.Ni wabunge ambao muda wao mwingi wa mapumziko wamekuwa wakiutumia kukijenga chama.Ni mfano wa kuigwa kwa wabunge hawa na wengine wanapaswa kufuata mfano huu.
 
Nimekuwa kila siku nahoji hivi Zitto naye angekuwa anafanya kazi kama hawa Majembe, CCM ingekuwa na pakushika?
 
Kazi ya Vicent kwa chama ni kubwa kiasi kwamba hapa Musoma wanaanza kuona kama amewatelekeza wananchi wake kumbe ni busy na shughuli za ujenzi wa chama. Jembe Vicent kaza buti ila ukumbuke na kuwavisit watu wako wa Nyasho, Nyakato, Buhare, Kamunyonge, Kitaji, Mukendo etc...pamoja sana
 
Mungu awasaidie waendelee kutoa elimu ya kutosha ili iwe raisi kuing'oa CCM!
 
Back
Top Bottom