Lema kuandaa maandamano makubwa jijini Arusha

Lema kuandaa maandamano makubwa jijini Arusha

Alvin Slain

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
6,375
Reaction score
3,668
Mjumbe wa kamati kuu ya chadema na aliyekuwa mb wa arusha mjini GODLESS LEMA Amesema ataandaa maandamano makubwa jijini arusha kutaka watu wote waliomo magerezani mkoani humo wanaokabiliwa na wizi wa kuku,sigara,ubakaji,ujambazi, na wahalifu wote kuachiwa huru iwapo serikali ya CCM haitawafikisha mahakamani mawaziri waliojiuzulu na wanaodaiwa kutafuna zaidi ya bilion 9 mali ya umma.
 
wafungwa wote waachiwe na waombe msamaha kama ambavyo tunaona watuhumiwa hawafikishwi mahakamani
 
alisema wafungwa wajiuzulu kuiba halafu waachiwe huru sababu wezi serikalini wanajiuzulu kesi zinaisha.
 
Aache ujinga kwani maandamano mpaka arusha tuu?Aandae singida au moro
 
Huyu naona hanazo.
Majambazi na wahalifu waachiwe???
Angeongea kingine, but hapa katokota. Hamnaga shinikizo la kihivyo.
 
Mkuu Lema hawezi kuropoka hivyo ni mtu wa kufikiria acheni kumsingizia bana.Majambazi waachiwe mhhh
 
mmmh....hapa kuna utata kidogo.....kwani sheria inasemaje...?
 
Huyu naona hanazo.
Majambazi na wahalifu waachiwe???
Angeongea kingine, but hapa katokota. Hamnaga shinikizo la kihivyo.

yupi jambazi,aliyeiba mabilioni ya wananchi au aliyeiba kuku?
 
Anaandaa maandamano majambazi,wezi,wabakaji waachiwe!!!!!!!????

peoples pawa.......
 
Hakuna utata, ndio uwezo wake mh ulipofikia na pia inasemekana wengi wa hao "majambazi" ni maswahiba zake.

watch out!

kwani wewe hakuna jambazi wa kuiba sufuria ama kuku aliyefungwa ambaye ni jirani yako..utakuwa unaishi angani.GO LEMA GOOO.m2 anaiba kuku anaitwa jambazi...akina MAIGE tuwaitaje? Kidumu chama cha majungu
 
Hakuna utata, ndio uwezo wake mh ulipofikia na pia inasemekana wengi wa hao "majambazi" ni maswahiba zake.

watch out!

Acha uwongo!Lema Godbless anauchungu na raia wanaoteseka gerezani wakati kesi zao ni ndogo na kuna mafsadi wameiba pesa za serikali mabilion.
 
Sasa tutafanyaje kama majambazi(mafisadi) hayafikishwi maakamani?
 
Huyu naona hanazo.
Majambazi na wahalifu waachiwe???
Angeongea kingine, but hapa katokota. Hamnaga shinikizo la kihivyo.

Mbona akina Mahige na wengine wengi tu wameachiwa.., Na hapo tuseme Magamba walitokota??
 
Back
Top Bottom