Lema aungana na ACT Wazalendo kwenye mkutano mkuu wa kidemokrasia wa miaka 50 ya Azimio la Arusha

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
.Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe Godbless Jonathan Lema ameungana na ACT Wazalendo kwenye mkutano mkuu wa kidemokrasia wa miaka 50 ya Azimio la Arusha .


UPDATES.
, ''Chombo cha habari kinapovamiwa tulitegemea kuona Rais Anachukua hatua lakini badala yake yeye ndio anazidi kuvitisha'
Hamna rais wetu ambaye ameshawahi kuteua kaimu jaji mkuu, jiulizeni kwanini sasa hivi ameteuliwa kaimu? -
: Rais anasema kuna watu wanamkwamisha, Mimi nasema Adui wa Rais Magufuli ni Rais Magufuli -
Hakuna namna zaidi ya kumdhibiti Rais Magufuli Kwa kumwajibisha KIKATIBA
'-Zitto Kabwe,mkutano wa Kidemokrasia Arusha.
tmp_11897-IMG_20170325_14342919411654.jpg

tmp_11897-IMG_20170325_143433329971433.jpg

==================
Wafanyakazi wa Tanzania wananyonywa mpaka damu

Zitto Kabwe, MB
25/3/2017
Hapa nchini kwetu, kama tulivyoonyesha takwimu hapo juu, Wafanyakazi kwenye sekta rasmi ni milioni 2.1 sawa na asilimia 9 tu ya nguvu kazi yote ya Taifa. Hawa wameajiriwa kwenye sekta binafsi (1.4m sawa na 67% ) na sekta ya umma (700,000 sawa na 33%). Hawa wanalipwa mishahara na posho mbalimbali kama chanzo cha mapato yao. Asilimia 91 ya Watanzania wapo kwenye sekta isiyo rasmi na rekodi ya mapato yao yaweza kuwa kizungumkuti kuipata. Hata hivyo tunajua kuwa wengi wameajiajiri wenyewe kwenye kilimo na biashara ndogo ndogo, uvuvi, ufugaji, uchimbaji wa madini na utoaji huduma. Ni muhimu kusisitiza kuwa Watanzania wengi hawamo kwenye ajira rasmi au isiyo rasmi. Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa ya mwaka 2015 inaonyesha kuwa Jijini Dar es Salaam kwa mfano ni asilimia 60 tu ya wakazi wake wapo kwenye ama ajira rasmi au ajira isiyo rasmi na asilimia 40 hawana kazi yeyote.
Uchambuzi pekee ambao tunaweza kuufanya kwa sasa ni kwa kutumia vyanzo vya mapato ya serikali ambapo tutaona mchango wa kaya kwenye mapato ya Serikali kulingana na vyanzo yake vya mapato.
Kwa mfano, Kitabu cha Mapato ya Serikali Kuu cha mwaka 2016/17 kinaonyesha kuwa Wafanyakazi wote wa sekta ya Umma na Sekta Binafsi watachangia jumla ya shilingi trilioni 3 kwenye mapato yote ya Serikali kulinganisha na wenye mitaji ambao watachangia jumla ya shilingi bilioni 900 tu kutoka kwenye kodi za faida/gawio, ongezeko la mitaji na riba (taxes on income/interests, profits and capital gains ).
Hata ukitazama miaka miwili ya nyuma utaona kwammba mwaka 2015/16 makampuni yalichangia shilingi 773 bilioni wakati Wafanyakazi walichangia 2.2 trilioni na mwaka 2014/15 makampuni yalichangia 600 bilioni na wafanyakazi 1.9 trilioni kama kodi zao kwenye mapato ya Serikali. Kwa kutumia kigezo cha Kodi za Mapato, matajiri wanachangia robo tu ya mapato yote ya serikali na wafanyakazi wanachangia robo tatu iliyobakia. Hii inachangia sana kuwepo kwa tofauti ya kipato ndani ya jamii.
Kwanini wafanyakazi wanachangia zaidi kuliko wenye mitaji ni swali ambalo tutalieleza. Sababu kubwa ni kuwa mabepari wana fursa ya kukwepa kodi kisheria wakati wafanyakazi hawana uwezo huo. Kodi za wafanyakazi hukatwa moja kwa moja na waajiri kutoka kwenye mishahara yao.
Kwanini Kodi za Makampuni ni kidogo kuliko za Wafanyakazi?
Wafanyakazi wa hukatwa kodi zao kutoka kwenye mishahara yao moja kwa moja ikiwemo pia makato mengine kama michango kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Bima ya Afya. Makato hayo huanzia asilimia 9 kwa mishahara ya ngazi ya chini mpaka asilimia 30 kwa wenye kulipwa mishahara ya juu kabisa. Kwa hiyo kodi ya wafanyakazi ni kodi ambayo serikali ina uhakika nayo moja kwa moja. Kwa takwimu ambazo tumeziona tayari, ni wafanyakazi wa sekta rasmi tu ndio hubeba mzigo wote wa kodi za wafanyakazi hapa nchini. Lakini kwanini kodi zinazotokana na mapato ya makampuni ziwe kidogo kuliko kodi zinazotokana na mapato ya wafanyakazi?
Kwenye makampuni, Kodi ya Mapato ni asilimia 30 ya faida ambayo kampuni imepata. Lakini mapato yanayokusanywa kwenye kodi hii ni kidogo sana kama tulivyoona, shilingi bilioni 600 tu kati ya mapato yote ya serikali mwaka 2016/17 sawa na asilimia nne tu ya mapato yote ya serikali yanayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania. Hali halisi hii sio ya Tanzania peke yake.
Mwanazuoni Thomas Piketty anaeleza kuwa “ ingawa kodi za faida za makampuni ni kati ya asilimia 40-50 kwenye nchi za magharibi, mapato kwenye kodi hizi hayazidi asilimia 2.5-3 ya Pato la Taifa”. Piketty anaendelea kuandika kuwa “ nadharia ya faida inayotozwa kodi ni nyembamba kuliko nadharia ya mapato ghafi ya ziada kwa sababu makampuni huondoa gharama za uchakavu wa mitambo, riba kwa mikopo na hata gharama za bima.
Kodi kwenye faida imegubikwa na matundu mengi kwenye mfumo mzima wa kodi duniani” (msisitizo ni wangu). Matundu haya ndiyo njia za ukwepaji kodi zinazofanywa na makampuni na hasa makampuni ya kimataifa ( Multinational Corporations ). Nchi za Afrika zimeathirika mno na mfumo wa kodi wa kimataifa na hivyo kupelekea fedha nyingi kutoka Afrika kutoroshwa kwenda ughaibuni.
Azimio la Tabora limeeleza kidogo kadhia hii ambayo Serikali za Afrika hazitilii maanani kabisa licha ya taarifa nzuri ya Rais mstaafu Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini. Ninanukuu “Katika kitabu cha ‘Africa’s Odious debts: How foreign loans and capital flight bled a continent’, waandishi Leonce Ndikumana na James Boyce, wameonesha kwamba katika kipindi cha miaka 40 iliyopita, jumla ya dola za Kimarekani bilioni 11.4 zimetoroshwa kutoka Tanzania kwa njia mbalimbali.
Hizi ni sawa na wastani wa dola za Kimarekani 285 milioni kutoroshwa kila mwaka kuanzia mwaka 1970 mpaka 2010. Sehemu kubwa ya fedha hizi zinatoroshwa na makampuni makubwa ya kigeni yanayofanya biashara na kuwekeza hapa nchini”.
Africa Progress Panel na kikosi kazi kilichoongozwa na Rais Thabo Mbeki ilieleza kuwa Afrika hupoteza zaidi ya dola za kimarekani bilioni 50 kila mwaka kutokana na utoroshaji wa fedha unaofanywa hususan na makampuni haya ya kimataifa.
Inasemekana asilimia 30 ya utajiri wa fedha wa bara la Afrika umewekwa kwenye pepo za kodi (tax havens ) kwa mujibu wa kitabu cha The Hidden Wealth of Nations kilichoandikwa na Gabriel Zucman, mhadhiri wa London School of Economics.
Katika kitabu hicho, Zucman ameonyesha takwimu kutoka Benki ya Taifa ya Uswisi zinazothibitisha kuwa takribani dola za kimarekani bilioni 150 kutoka Afrika zimehifadhiwa kwenye mabenki ya nchi hiyo. Jumla ya Pato la Taifa (GDP) ya nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki ni dola za kimarekani 147.3 bilioni, hivyo fedha za Afrika zilizopo Uswisi ni zaidi ya GDP ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kwa pamoja. Fedha hii ni mara tano ya gharama za kujenga mradi wa Inga Dam kule Kongo ambao ungeweza kuzalisha umeme wa kutosha bara zima la Afrika.
Pamoja na mambo mengine, matundu haya ya ukwepaji kodi yamejengwa ndani ya mfumo wa kodi za kimataifa. Kuna kitu kinaitwa kwa lugha ya kigeni Base Erosion and Profit Shifting ikiwa na maana kuwa makampuni ya kimataifa yanapowekeza hapa nchini huhamisha faida kupeleka nchi zenye viwango vidogo vya kodi na hivyo kutolipa kabisa kodi hapa nchini ama kulipa kodi kiduchu sana.
Kwa mfano, katika kukokotoa kodi kampuni huondoa gharama za riba za mikopo, bima na gharama za utawala na kinachobakia ndio faida ambayo hutozwa kodi. Kampuni hizi huchukua huduma hizi za mikopo, bima na utawala kutoka kwa makampuni dada na kuongeza gharama maradufu na hivyo kuhamisha fedha hizi kana kwamba wanalipia hizi gharama na hivyo kupunguza sana wigo wao wa kodi. Ndio maana siku za nyuma tulisikia kampuni za madini hazilipi kodi ya mapato kwa sababu nyingi zilikuwa zikitumia mtindo huu wa kumomonyoa wigo wa kodi.
Wakati nikiwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Madini ya Jaji Mark Bomani tulikuta ushahidi wa kampuni ya Geita Gold Mines ambayo uwiano wa mtaji wake na mikopo (debt-equity ratio) ulikuwa asilimia milioni 12. Hii iliifanya kampuni hii kumomonyoa kila walichokipata katika uchimbaji wa dhahabu nchini kwetu na kukihamishia njia kana kwamba ni malipo ya mikopo waliyochukua kumbe ni mbinu ya kukwepa kodi na kupora dhahabu ya Tanzania.
Nilipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, tuliagiza ukaguzi wa ukwepaji kodi unaofanywa na makampuni ya kimataifa na iligundulika kuwa karibia kila sekta ya uchumi ilihusika na ukwepaji kodi.
Mfano ambao huwa naukumbuka mara kwa mara ni mfano wa mauzo yetu ya Korosho kwenda nje. Hupenda kuurudia na nitaurudia tena hapa.
Mwaka 2011 Tanzania iliuza Korosho kwa nchi ya India. Kwenye rekodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania ilionyesha kuwa tuliuza tani 80,000 za korosho kwa bei ya dola za marekani 1000 kwa kila tani sawa na dola za kimarekani 80 milioni.
Uchunguzi ulionyesha kuwa katika nchi ya India rekodi yao ya Korosho walizonunua kutoka Tanzania ilikuwa ni dola za kimarekani 120 milioni kwa sababu wao walinunua tani 120,000 za korosho kutoka Tanzania. Hii ina maana kuwa tani 40,000 hazikurekodiwa kwenye forodha zetu na hivyo wauzaji kukwepa kodi ya ushuru wa korosho wa zaidi ya dola za kimarekani 12 milioni.
Pia kwenye kodi ya Mapato ya kampuni iliyouza korosho hizi mapato ya zaidi ya dola 40 milioni hayatoonekana na hivyo kufanikiwa kukwepa kodi. Huu ni mfano ninaopenda kuuleza katika kueleza namna mfumo wetu wa kodi ulivyojaa matundu na kuhitaji kufanyiwa kazi kubwa ya kuufumua.
Kwa hiyo makampuni yana njia nyingi za kukwepa kulipa kodi na hivyo wamiliki wake kujilimbikizia mali nyingi na kuongeza tofauti ya kipato miongoni mwa wananchi. Kama hatua madhubuti hazitachukuliwa tofauti ya kipato itazidi kuongezeka na kuleta hatari kubwa kwa ustawi wa wananchi na usalama wa nchi yetu.
Moja ya suala ambalo chama cha ACT Wazalendo ililieleza na halikuelezwa na chama kingine chochote katika kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ilikuwa ni hili la kufanya marekebisho ya mfumo wa kodi ili kila anayepaswa kulipa kodi alipe kwa haki na kwa uwazi. Tuliahidi “ kuweka mfumo mpya wa kodi za kimataifa ili kuzuia makampuni ya kimataifa kumomonyoa wigo wa kodi kwa kushiriki kikamilifu katika kampeni za kimataifa za kurekebisha mfumo wa kodi za kimataifa, kupitia mikataba ya kikodi na nchi nyengine ili kuzuia ukwepaji kodi na kujengea uwezo kitengo cha kodi za kimataifa ili kudhibiti ukwepaji kodi”.
Serikali ya Awamu ya Tano imefanya nini katika eneo hili?
Serikali ya Awamu ya Tano ilisifika kwa makusanyo makubwa ya kodi katika miezi yake ya mwanzo ya kuongoza nchi yetu. Lakini haijafanya juhudi yeyote ya ndani au ya nje kuhakikisha kuwa nchi inaondoa tofauti kubwa ya kipato kati ya wenye nacho na wasio nacho. Mara kadhaa Rais wa Jamhuri ya Muungano amekuwa akisikika kusema kuwa “anataka waliokuwa wanaishi kitajiri waishi kishetani”.
Sina hakika kama hili ni jambo la mantiki katika kufumua mfumo wa uchumi ili watu wengi zaidi waweze kuondoka kwenye umasikini. Juhudi za kuendesha kampeni ya kimataifa ili kuboresha mfumo wa kodi za kimataifa zimeshuka chini na kiukweli kama nchi tumerudi nyuma wakati dunia nzima inashiriki kwenye kampeni hizi. Juhudi za ndani za kuongeza makusanyo ya kodi kama hazitatazama mfumo wa kodi za kimataifa, basi hazitakuwa na faida yeyote na tutabakia na kodi za wafanyakazi na vibarua tu kuendesha nchi yetu. Tunaendelea kinyume kinyume, kwamba Pato la Taifa linakua kwa kasi lakini 1) Idadi ya Watanzania masikini inaongezeka na 2) Tofauti ya kipato miongoni mwa wananchi inaongezeka kwa matajiri kuwa matajiri zaidi na masikini kuwa masikini zaidi
 
.
Chombo cha habari kinapovamiwa tulitegemea kuona Rais Anachukua hatua lakini badala yake yeye ndio anazidi kuvitisha''-Zitto Kabwe,mkutano wa Kidemokrasia Arusha,25 Machi 2017
 
.Hamna rais wetu ambaye ameshawahi kuteua kaimu jaji mkuu, jiulizeni kwanini sasa hivi ameteuliwa kaimu? -Zitto Kabwe
 
.Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe Godbless Jonathan Lema ameungana na ACT Wazalendo kwenye mkutano mkuu wa kidemokrasia wa miaka 50 ya Azimio la Arusha .

=================
UPDATES.
, ''Chombo cha habari kinapovamiwa tulitegemea kuona Rais Anachukua hatua lakini badala yake yeye ndio anazidi kuvitisha''-Zitto Kabwe,mkutano wa Kidemokrasia Arusha,25 Machi 2017

Zzk kijana acha kutumika, umeshikia bango kutetea wazungu wa unga mpaka unakosa muda wa kunyoa midevu! Povu la nini haswa? Rais keshasema hapangiwi na kuteua na kutengua ni uamuzi wake!
 
.Makampuni makubwa na haswa makampuni ya uwekezaji yanakwepa sana kodi.Lakini wafanyakazi rasmi wanalipa sana kodi @zittokabwe [HASHTAG]#AzimoLaArusha[/HASHTAG]
 
.Mashirika ya Umma kwa sasa e.g. Tanesco sio mashirika ya umma ni mashirika la serekali...kuna tofauti. Ni ubepari wa kidola @zittokabwe
 
Hao azama wanataka kuvamiwa au hawajui kuwa hii ni Dar ya bashite na baba yake
 
.Serikali ya Awamu ya Tano ilisifika kwa makusanyo makubwa ya kodi katika miezi yake ya mwanzo ya kuongoza nchi yetu. Lakini haijafanya juhudi yeyote ya ndani au ya nje kuhakikisha kuwa nchi inaondoa tofauti kubwa ya kipato kati ya wenye nacho na wasio nacho. Mara kadhaa Rais wa Jamhuri ya Muungano amekuwa akisikika kusema kuwa “anataka waliokuwa wanaishi kitajiri waishi kishetani
 
Adui wa magu ni magu mwenyew
Hii nimeipenda mwambien aache kulalamika achape kazi
Na asitupangie cha kusema
 
Back
Top Bottom