Lema atinga bungeni, achafua hali ya hewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lema atinga bungeni, achafua hali ya hewa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Nov 17, 2011.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Mwananchi

  Wednesday, 16 November 2011 21:15
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Habel Chidawali, Dodoma

  MBUNGE wa Arusha Mjini Godbless Lema (Chadema) jana alichafua hali ya hewa wakati akiingia katika ukumbi wa bunge baada ya wabunge wa chama chake kumshangilia bila utaratibu kwa kugonga meza na kuvuruga ratiba nzima.Lema aliingia bungeni saa 3:37 asubuhi akiongozana na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na kushangiliwa na wabunge wa Chadema na kusababisha kelele.

  Wakati Lema akiingia, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Lazaro Nyarandu alikuwa akijibu swali namba 88 lililoulizwa na Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi) na kushindwa kuendelea kutokana na kelele hizo na kusimama kwa muda.
  Lema hakuwapo wakati mkutano wa tano wa bunge ulipokuwa unaanza wiki lililopita baada ya kuwa rumande katika Gereza la Kisongo, nje kidogo ya Jijini la Arusha kutokana na kufanya mkusanyiko bila kibali.

  “Waheshimiwa wabunge kwani kuna nini, mbona kelele ni nyingi hebu tulieni basi tumsikilize Naibu Waziri, waheshimiwa wabunge utulivu tafadhali,’’ alisikika Mwenyekiti wa Bunge Jenister Mhagama akisema katika kikao cha asubuhi.
  Pamoja na kuonywa na Mwenyekiti huyo, wabunge wa Chadema hawakusitisha kelele na waliendelea kugonga meza kwa furaha mpaka Lema alipoketi katika kiti chake.

  Baada ya Lema kuketi kwenye kiti chake, Naibu Waziri aliendelea kujibu swali la Mkosamali.
  Mbali na Lema, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Athuman Mfutakamba jana alilishangaza Bunge baada ya kuitwa kujibu swali namba 96 huku akiwa nje.
  Swali la Vincent Nyerere (Musoma Mjini-Chadema) lilisababisha Mfutakamba kuingia ukumbini mbio ili kulijibu, lakini alichelewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi aliamua kujibu.

  Naye Suzy Butondo kutoka Shinyanga kwamba Mahakama ya Hakimu mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Shinyanga imemsimamisha kizimbani mbunge wa Chadema wa Jimbo la Meatu, Meshack Opulukwa na viongozi wenzake wawili wa Wilaya ya Meatu kwa kufanya mkutano wa hadhara kinyume na amri ya polisi.

  Mbunge huyo alisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Shinyanga John Chaba ambaye alizuia mikutano ya Chama hicho ndani ya Jimbo la Meatu ambayo ililenga kuwashukuru wananchi kwa kumchagua.

  Washtakiwa wote walikana mashtaka na kufafanua kwamba
  walikuwa na kibali halali cha kufanya mikutano hiyo. Washtakiwa hao wako nje kwa dhamana na itaendelea Desemba 6, mwaka huu.

  Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Na bado! mapambano ndiyo yanaanza!
   
 3. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Swafiiiiiiiiiiiii jamaa mapovu yanawatoka kama hili linavyoongea hv sasa.
   
 4. N

  NnyaMbwate JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,404
  Likes Received: 532
  Trophy Points: 280
  Uandishi mwingine jamani Looh! Hivi Kumshangilia Shujaa ni kuchafua hali ya hewa? Na hao wasema mipasho si ndo wachafuzi wa hali ya hewa kwetu sisi tulowapeleka bungeni! IMBOMBO JH'ILIPO!!
   
 5. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Mpaka wakome mwaka huu wataishia kutapatapa hivihivi
   
Loading...