Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema(CHADEMA), amelitaka Bunge kuvunja Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kutokana na maoni ya kambi hiyo kutosikilizwa.
Aidha, lema amedai kuna kuchujwa kwa maneno yanayochangiwa na wabunge wa kambi hiyo katika mijadala katika kumbukumbu za Bunge(Hansard) alikodai kunafanywa na wafanyakazi wa Studio ya Bunge.
Aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana asunuhi aliposimama na kuomba mwongozo wa Kiti cha Spika akidai kuwa michango ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imekuwa ikihaririwa na baadhi ya maneno yamekuwa yakiondolewa na hivyo kutorushwa kwenye studio hiyo na hata kwenye taarifa wanazopewa waandishi wa habari wa redio na televisheni.
Hata hivyo, katika mwongozo wake kuhusu suala hilo muda mfupi kabla ya kuahirisha shughuli za Bunge jana mchana, Mwenyekiti wa Bunge, Najma Murtaza Giga, aliyekuwa akiongoza kikao cha jana alisema Studio ya Bunge haina utaratibu wa kuchuja michango ya wapinzani isipokuwa kwa maelekezo ya Kiti cha Spika.
Katika hoja yake, lema alisema ni bora Bunge lingetoa mwongozo wa kuivunja Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni na lisipokee tena maoni yoyote kutoka kwao kutokana na maoni yao kutosikilizwa.
"Mheshimiwa Mwenyekiti mimi nimechangia Wizara ya Mambo ya Nje na (Ushirikiano wa) Afrika Mashariki, nikaenda nikaambiwa nijaze fomu, nimejaza kutaka kumbukumbu ya mchango wangu, mchango ambao haukuwa hata na mwongozo, haukuwa na taarifa wala utaratibu(bungeni)"
" Nimekwenda mambo yote yanayohusu mambo ya Acacia na Diplomasia ya Uchumi yametolewa, wamenibakizia pale panaposema tu mtu yeyote anayepinga rasilimali ni mwendawazimu na kipande hicho ndiyo kinazungushwa"
Akijibu hoja hiyo, Mwenyekiti Giga alijibu kama ifuatavyo
"Kilichotokea kwa mchango wa Lema ni kosa la kiufundi na linafanyiwa kazi na likitatuliwa anaweza kuomba kupewa mchango wake wote"
Giga aliongeza kuwa mbunge yeyote atakayekumbana na changamoto kama iliyompata Lema awasilishe malalamiko yake kwenye Ofisi ya Katibu wa Bunge.
Chanzo: Nipashe