Lema apinga kugawana vyeo, hamtambui naibu meya wala meya wa Arusha (tamko)

Hee sasa kama Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa hajui muafaka huu muafaka ulifikiwaje? Pia najiuliza mbona taarifa imetolewa na Lema kisha ndio Mbowe anasema hatambui muafaka? Huu muafaka tumeusikia kama siku tatu hivi zilizopita mbona uongozi wa CHADEMA Taifa ulikuwa kimya hadi Lema atoe taarifa kama Lema na wala si taarifa ya Chama? Kuna mengi ya kujiuliza hapa.
 
Tunachosubiri ni kusambaratika na ngumi zipigwe CDM dhambi za udini zinawatafuna
 
Mbowe amesema yeye na Uongozi wa juu wa Cdm haumtambui meya wala naibu wake na wanafanya uchunguzi nini kilitokea kikapelekea muafaka huo batili.Mimi namhurumia Regia Mtema aliyekuwa anatumia nguvu nyingi hapa JF kuutetea Muafaka huo. kweli Viti Maalum ni mzigo kwa taifaSource: TBC 1-Habari
 
Tunachosubiri ni kusambaratika na ngumi zipigwe CDM dhambi za udini zinawatafuna

Mkuu ngumi hazijengi ila hapa naona Lema kakasirika! Huenda akatoa ile kauli ya milango ifungwe tupigane siku CHADEMA ikiketi kuongelea hili suala.
 
Naomba wana JF mnijibu hayo mapatano baina ya CDM na MAGAMBA yalifanyika chini ya viongozi gani wa CDM mbona hatuwaelewi hawa CDM. Je Lema alishirikishwa na viongozi wenzake wa CDM au la?????????
 
nimetoka kusikiliza habari tbc ya saa 2 usiku, lema ametangaza hamtambui naibu meya, mbowe ameongea lkn kama kawaida ya tbc walimkata baada ya sec kama 10 hivi lkn alichokiongea mbowe ni kama na yeye pia ameshangazwa na kilichotokea ktk ndoa na magamba i mean hata yeye ni kama hajui kilichoendelea arusha
 
Hapa ndipo CHADEMA inapolaumiwa hasa kwenye eneo la utoaji taarifa kwa umma. Wengi sana humu JF wamewahi kuhoji kama chama kinayo Ofisi/Kitengo cha mahusiano ya umma na kama kipo kinafanya kazi zake sawasawa. Haiwezekani masuala mazito kama haya hakuna taarifa rasmi za uhakika kutoka kwa wahusika. Unategemea taarifa kama hizi gazeti la Uhuru au Habari Leo kwa mfano liandikeje? Leo humu humu JF Mh. Lema katoa taarifa yake kupinga mwafaka huo mara hii tena Mwenyekiti anadaiwa kuzungumza mengine; uhakika ni upi? Hebu Ofisi inayohusika wekeni taarifa rasmi na msimamo wa chama kwenye website ya Chama.
 
nimetoka kusikiliza habari tbc ya saa 2 usiku, lema ametangaza hamtambui naibu meya, mbowe ameongea lkn kama kawaida ya tbc walimkata baada ya sec kama 10 hivi lkn alichokiongea mbowe ni kama na yeye pia ameshangazwa na kilichotokea ktk ndoa na magamba i mean hata yeye ni kama hajui kilichoendelea arusha

Mkuu nimemsikiliza amesema kwamba yeye kama mwenyekiti wa Taifa haujui huo muafaka na wanafanya uchunguzi kubaini nini kilitokea. Ila jambo la kushangaza ni kwamba mbona siku kama nne zimepita bila uongozi wa CHADEMA Taifa kutoa taarifa kukanusha muafaka huu hadi Lema ametoa Taarifa tena kama Lema si Chama ndio Mbowe naye anasema hautambui huu muafaka? Kuna kitu hapa ambacho hatuambiwi. Kwa mujibu wa Report ya Lema naona yeye ndio hautambui huu muafaka si Chama. Ila kabla jogoo hajawika ukweli utakuwa umeishajulikana.
 
So waliokaa kule Arusha wakafikia muafaka wanatoka chama gani?
au kikao kile hakikua na baraka za uongozi wa juu?
 
Chama hakiwezi kutoa taarifa kwa kukurupuka kwanza uchunguzi juu ya maamuzi ya Arusha unafanyika kwa umakini giza lote litaondolewa
 
Hii issue ya Mayor wa Arusha inaonekana kuzua maswali mengi zaidi. Mh Mbowe ameonekana TBC1 (8pm news bulletin) akisema kuwa yeye kama kiongozi wa kambi ya upinzani hana taarifa za muafaka wa u-mayor Arusha ila amesikia hayo kwenye vyombo vya habari. Pia anasema Mbowe, uongozi wa juu wa CHADEMA nao hauna taarifa. Sasa ni nani alifanya maazungumzo ya muafaka?

Hivi inawezekana kweli ccm walikaa na madiwani wachache wa CHADEMA-arusha mjini (a) bila mbunge wa arusha kama mjumbe kwenye baraza la madiwani kujua? na (b) bila ya uongozi wa Taifa -CHADEMA kujuwa? Kama kweli ccm wamefanya hivyo kuna tofauti gani na ujangili? mambo ya kitoto kabisa haya!
 
Mbowe msanii sana anachezea akili za pro-CDM. Wakati yeye mwenyewe kakaa kikao na Pinda, Ahahahaha!!
 
Ni kweli nimemuona Mbowe TBC1 (8pm news bulletin) akisema kuwe yeye kama kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni hajui huu muafaka wa Arusha, na wala uongozi Taifa wa CHADEMA hawajui chochote kuhusu huo muafaka! Je ni nani ali-sign muafaka Arusha, na pili kwa nini imewachukuwa CHADEMA 'days' kutoa kauli ya kupinga taarifa za kuwepo muafaka?

Hata hivyo nawatabiria CHADEMA kuibuka kidedea kwenye huu 'mchongo' wa kurubuni watu kwa vyeo!
 
waliokaa ni madiwani wa ccm tlp na cdm , ila maamuzi hayana baraka za chama (cdm)
Ritumeelewa? Maongezi level ya taifa yalikuwa yatolewe uamuzi
July mosi sasa imeshakuwa haifai tena
 
Back
Top Bottom