Lema apewa chopa kujenga Chadema

Lema apewa chopa kujenga Chadema

EasyFit

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Posts
1,269
Reaction score
1,082
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimempatia aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, helikopta na vifaa vingine kuzunguka nchi nzima kuhamasisha wananchi kukiunga mkono chama hicho, wakati huu ambapo anasubiri maamuzi ya Mahakama ya Rufaa kuhusu kuenguliwa ubunge wake.

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, alipokuwa akihutubia umati wa watu uliofurika katika uwanja wa Barafu Dodoma jana.

"Ninajua mna hamu ya kusikia kuhusiana na mbunge wenu Lema, (wananchi wanaitikia ndiyo), tumempatia kazi maalum kwa kumpa helikopta, muziki mkubwa na matarumbeta," alisema.

"Anakwenda kuamsha ari ya mageuzi nchini, hakuna kulala hadi kieleweke. Wangejua ni balaa kwa hili walilolifanya wangemuacha bungeni," aliongeza Mbowe huku akishangiliwa na umati wa watu.

Gazeti la Nipashe.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimempatia aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, helikopta na vifaa vingine kuzunguka nchi nzima kuhamasisha wananchi kukiunga mkono chama hicho, wakati huu ambapo anasubiri maamuzi ya Mahakama ya Rufaa kuhusu kuenguliwa ubunge wake.

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, alipokuwa akihutubia umati wa watu uliofurika katika uwanja wa Barafu Dodoma jana.

“Ninajua mna hamu ya kusikia kuhusiana na mbunge wenu Lema, (wananchi wanaitikia ndiyo), tumempatia kazi maalum kwa kumpa helikopta, muziki mkubwa na matarumbeta,” alisema.

“Anakwenda kuamsha ari ya mageuzi nchini, hakuna kulala hadi kieleweke. Wangejua ni balaa kwa hili walilolifanya wangemuacha bungeni,” aliongeza Mbowe huku akishangiliwa na umati wa watu.

Gazeti la Nipashe.

pamoja na tunaimani na kamanda Lema
 
Yap!The ball is rolling on our side PEOLES POWEEEEEEEEEEEEEEEER!!!
 
Safi sana Cdm. Magamba watatamani Lema arudi Bungeni na jinsi alivyo na mvuto kila kona ya nchi ndio ataita hisia za watu kujua haki zao kwa unasaha. CDM mmebuni kitu kizuri sana. Hatukiwii kusikia na mikutano ya hadhara imekatazwa nchi nzima.
 
Tatizo la CCM ni kufanya kazi kwa matukio hawaangalii zaidi ya hapo, kuwa hili walichoangalia ni ku-neutralize furaha ya ushindi wa Arumeru Mashariki, kama walivyopiga marufuku mikutano Dodoma baada tu ya CDM jana kuitikiwa na watu. Sasa kazi inayofuata ni kuanza kumfuatilia Lema popote atakapo kwenda. Kuna wengine walifikia kusema ukimpiga teke chura unamsaidia mwendo.
 
Hakuna kulala mpaka kieleweke,yaani hapo CHADEMA wamewapiga CCM bao la kisigino,magamba wamefanya one mistake lakini wamepigwa 2 goals.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimempatia aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, helikopta na vifaa vingine kuzunguka nchi nzima kuhamasisha wananchi kukiunga mkono chama hicho, wakati huu ambapo anasubiri maamuzi ya Mahakama ya Rufaa kuhusu kuenguliwa ubunge wake.

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, alipokuwa akihutubia umati wa watu uliofurika katika uwanja wa Barafu Dodoma jana.

“Ninajua mna hamu ya kusikia kuhusiana na mbunge wenu Lema, (wananchi wanaitikia ndiyo), tumempatia kazi maalum kwa kumpa helikopta, muziki mkubwa na matarumbeta,” alisema.

“Anakwenda kuamsha ari ya mageuzi nchini, hakuna kulala hadi kieleweke. Wangejua ni balaa kwa hili walilolifanya wangemuacha bungeni,” aliongeza Mbowe huku akishangiliwa na umati wa watu.

Gazeti la Nipashe.

Ajitahidi kupita kwenye ile mikoa migumu migumu tu! Kama Dodoma na maeneo mengine kama haya.Mpaka kieleweke.
 
...hawachelewi kuidungua.

Hawana ujanja huo, tumeshawazidi ujanja... mipnga yao chafu dhidi ya viongozi wa CDM tunaifahamu kabla hawajamaliza kikao husika cha utekelezaji wa mpango wa aina yeyote...

Hata kikao kikifanyika Ikulu tunajua.
 
Tatizo la CCM ni kufanya kazi kwa matukio hawaangalii zaidi ya hapo, kuwa hili walichoangalia ni ku-neutralize furaha ya ushindi wa Arumeru Mashariki, kama walivyopiga marufuku mikutano Dodoma baada tu ya CDM jana kuitikiwa na watu. Sasa kazi inayofuata ni kuanza kumfuatilia Lema popote atakapo kwenda. Kuna wengine walifikia kusema ukimpiga teke chura unamsaidia mwendo.
Chadema inapelekea watu wa Usalama wa Taifa waanze kutafuna per diem za kumfuatilia Lema mikoani. Kwa usalama wa Taifa wa hivi ni bora nchi isiwe na kitengo cha usalama wa Taifa, ni usalama wa Taifa gani una-deal na kufuatilia maandamano ya vyama huku Twiga wakisafilishwa kwa ndege kwenda nchi za nje bila kufuata taratibu? labda mimi sifahamu nini maana ya usalama wa Taifa.
 
Kwa lema hapo chadema ni nimewapenda.LEMA ANAMVUTO WA KIPEKEE.
 
Hongera sana Lema, hiyo ndiyo kazi saizi yako. Ubunge ulikuwa haukufai, kukupa ubunge wananchi wa Arusha waliku overdose.
 
Huwezi kujenga chama kwa Chopa ni matumizi mabaya ya pesa kuna mambo mengi ya msingi ya kufanya chama hakina ofisi mikoani hata makao makuu hali sio nzuri...mnawachangisha pesa wananchi halafu mnamkodishia Lema Chopa.

Tuwe wakweli hivi Lema ana Influence gani kwenye siasa za Tanzania?

Siasa za Lema ni sehemu za kaskazini maeneo ya Arusha, Kilimanjaro.
 
Back
Top Bottom