Ni miaka mingi imepita toka nifanye safari yangu ya mwisho kuja Dar es Salaam, nimeingia wiki iliyopita mambo mengi nimekuta yamebadilika ila lililonishangaza zaidi ni hali ya sasa ya viwanja vya leaders club pale kinondoni mitaa ya Ada estate ambapo pia matamasha mengi makubwa hufanyika, pamepooza sana yani bar yake imekufa, hakuna ma_bonanza tena
Nakumbuka pale palikuwa kila jumamosi hapatoshi maana palikuwa na bonanza la akina msondo ngoma ya akina tx moshi,ngulumo,mbwembwe nk na twanga pepeta ya akina choki,amigolasi nk nakumbuka nilikuwa sikosi kwa mchana na jioni nilienda pale victoria kwa maestro kikumbi mwanza mpango king kikii kumalizia siku kwa kupepelusha kitambaa cheupe na wazee sugu
Nilikuwa nikifanyia shughuli zangu mitaa ya kinondoni shamba na kila jion nilikuwa napitia pale kupata japo safari mbili ndipo niianze safar yangu kuelekea bunju, Bar ilipendeza sana japo uhuru ulikuwa finyu kias kwa maana maafisa wengi wa TISS walipenda kunywa pale so ilibidi tuwe makini na tunapozungumza
Eneo lile ni kubwa na potential sana kibiashara ila serikali (wameshindwa) kupatumia hivo ningeshauri kama inawezekana wampe muwekezaji apaendeleze maana tulizoea kuwa pale ndio sehem ya wastaarabu,nilienda nikapate kinywaji ila nlipofika ilibidi nicheke mzee mwenzangu Jangala ambaye ndiye meneja wa siku nyingi pale leaders club aliponambia bia mpaka anifatie sehemu..... Ilinibidi niende mahala pengine wanapaita 4ways park dah nilichokutana nacho ndicho kimenifanya niikumbuke leaders club yetu.
Ombi:utumishi ifufueni leaders club