Mi naamini kigezo pekee ili uwe mshindi ilikua ni kura
Diamond anaweza kuwa na followers wengi kwenye social media lakini wasimpigie kura kwa mambo mengi
Mosi, inawezekana zaidi ya robo tatu hao wafuasi wake ni kutoka nje ya nchi hivyo wasione umuhimu wa tuzo hizi au kukosa njia rahisi kuvote kama kutuma sms locally
Pili inawezekana wafuasi wake pia walibweteka wakajua atachukua tu bila ku play part yao ya kupiga kura
Tatu tuzo hizi haziangalii ubora wako upoje kwa sasa wak ni kura tu
Lakini pia mtu kulipia milioni tatu sio kigezo maana lets say Lundenga au madam Rita na hakika hana muda wa kupiga kura mara mia kwasababu alikipa milioni tatu lakini kuna msela kinyozi anaweza kumpigia Kiba kila siku kura za kumwaga
Ki msingi maamuzi ya jinsi hii hutatiza wengi kwasababu tunasukumwa na ama mahaba yetu binafsi au viashiria kwamba fulani anapendwa lakini mwisho wa siku fact ni vote ndio inaamua.
Ni mbaya kujiaminisha kuwa kwakuwa anajaza na kupenda ndio ushindi sababu kigezo ni kura
Kumbuka wema anawapenzi wengi sana, joketi halikadhalika na ile hali ya wafuasi wa kiba kunyanyasika na mafanikio ya chibu inaweza kuwapa msukumo wa kutuma sms nyingi saaaana maana upigaji kura ulikua hauna ukomo
So sioni akabu yoyote katika hali, tuzo zingine makini hawaangalii kura tu pekee wanaangalia na vigezo vingine ila hii ya watu waliachiwa watu wenyewe waamie