Lazy Billy Ataka Kuachwa Na GF baada ya 10 years. Agomaaa kuachwa katu na kutoa tamko zito kwa GF

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,700
29,116
Igweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kuna mdada anaitwa V, she is a snob and a half ndo kisa cha kutokua rafiki yangu. Ni mtu mwenye bahati ya maisha. Richa daddy, kamaliza chuo, straight As, big job, mzuri, sweet girl, her life is so perfect to make you envy her. I envy her too. Sasa ana high school sweet heart wake ambae ni LAZY BILLY mmoja balaaa. Walianzan toka Lazy Billy ni Aza boy. Wana almost 10 years together. Manake tokea form 5.

Lazy Billy ni mtu mwenye wazazi wanaojali watoto wao. Baada ya kutaga A level, akaenda Malasia, akala bata weeee, mpaka kuku wakaona wivu, akaja kwenda Seoul Korea huko ndo akarudi na Degree ya IT. Kusema kweli back in the days he was the coolest guy on the block. Ki A level, V asingeweza kumuacha hata nukta. He looks good, dresses good and humble too! Aaaaaw! the boy also knows how to have serious fun. Nakumbuka A level wenzie tulikuwa tunajiachia na watu wazimaa wako kazini, ukienda Le Bristol enzi hizo na jikaka lako, unamkuta Lazy Billy na kampani ya kufa mtu ya watoto wa Aza boys na Tambaza wanakula bata la maana sio la kubahatisha. Tena kunikomoa niko na jikaka langu afu watoto wlivokuwa washenzi wanatuma muhudumu atusikilize au wanatulipia bili. Mxiuuuuuuuu! Jikaka linanunaje, ndo vibwana vyako vile vya shule? Namzuga wale kaka zangu. Kila unakoenda mjini humu wapo, na first lady wao ambae ndio V sasa. V alipewa good times hakuna mfano.

Wanawake wanajitongozesha kwa Lazy Billy weee V yupo gado. The we grew up, non of that shit mattered any more ikawa maisha sasa. Chuo V alijiachia na several people lakini hakuna alieweza kufikia legacy ya Lazy Billy. So Lazy Billy alivorudi tokea Korea akakuta V ameajiriwa kama finance analyst wa avery reputable company mjini hapa. She was rolling big! Shule imemlipa. Lazy Billy katoka Korea, kazi hamnaa, washkaji wengi wamesepa all over the world, wazazi wamestaafu, akalamba joka. Akafanya juu chini wakarudiana na V sasa.

Well V was hopping Lazy Billy atapata kazi, wataoana maisha yataendelea. Akamkaribisha kwakwe akiwa anajipanga. Lazy Billy ni kushinda kwenye Tv, akitafutiwa kazi anataka alipwe 3m atleast. Bongo hiiii? Thubutuuuuu! He is angry, frustrated and bitter at life. Alivoona hapati ikaja V ampe mtaji 20m afanye biashara. V akakopa kweli hio hela akamgea. Hela ilipoyeyuka hakuna anaejua. V akamvumilia tu, anamlisha, anamvisha, anahudumia kwao, yaani hela za V ni hela zao wote wawili. Since 2011 mwendo ndo huo. Sasa 2014 akaamua awe promoter. Anaadaashow hizi za Ngwasuma Moshi, Arusha huko, hivo. Anafnya na dili zake zingine za matangazo mara kuandaa event za makampuni in short ANABANGAIZA TU kama Lara 1. And all this time V stood by him, hizo show zote anahudhuria, event zake anakaahad saa 9 na kesho ana wahi kazini. Awwww! So supportive of her.

V kafnya makeke, kaenda Nairobi kafanya mitihani ya CFA, kafaulu, kafanya ki MBA chake kapasi,yuko commited and dedicated kazini, Marshallah kaja bosi mpya kijana baada ya CFO mtu mzima kustaafu hio 2014. CFO is interested in V, kesha weka hilo crystal clear. V akamwambia tu niko comitted, aka insist He will wait,and gve her all the time she needs, aaaaaaaw!how sweet of him. Hio imefatana na wema uliozidi kipimo kuhakikisha bibie hachomoki kama kumuongezea Mshahara, mafuta litaza kutosha, OTza maana, kulipiwa ACCA, juzi jui kamwambia nataka ni create position ya Assistant Chief, special for you! I want to give you a career! Bi V ndo kubaki speechless.! Mbutananga! Ndo kujitetea we may never happen sijui nini, im still thinking about us, kimepanda nakushuka! CFO akamshush! Nimewahi kukuomba au kuku force unipe K? No! I am nice to you because i want to be nice you, it feels good to treat you nice. Kama utaamua kunilipa nuksani kwa hisaniyoote niliokufanyia and after everything i have done to you, i will forgive you from my heart. All i will ever do to you is be nice to you as much as i can. Mmmmmh! Makubwaaa!

Dunia ndogo taarifa za mi lunch ofisini na working late hours zikamfikia Lazy Billy. Weeeeeeeee! Lazy Billy kampa kubwa kamwambia swala la kuachana halipoooo! I have been your bich here for 4 years. Nimekuwa V's Bf, V's play toy, nimekuacha unikalie kichwani wee, yoote hio sababu nakupendaaa. We unafikiri ningeshindwa kwenda Dubai huko, Uk au Us kutafuta maishaaa? Sijaenda pamoja na mama na ndugu zangu kunisimamnga kila dakikaa because i love you and i want to spend my life with you hata kama hio itamanisha niwe nashinda hapa kwenye kochi kukusibiri utoke kazini. I have spent so much time of my life for you. Kwa hio kuachana hakupoooooo! I am your bich and you are my bich for life. Mi sikai hapa sababu una shingi 2 au 3, naweza kwenda Dubai kufanya maisha mwaka tu hunipati. Lakini all that will mean nothing kama hutokuwepo kwenye picha. Ukijaribu kuleta masihara na CFO matokeo yake yatakuwa TRAGIC. Tena kaa standby naenda kutoa mahri, tuoane hata saa 12 asubuhi, na naomba birth control iishe. Tunaanzisha familia. Kuachana haiwezekani, huwezi kunirudishia miaka yangu niliopotezaaa. Ukumbuke mimialwatanmjini hapa utaanzaje kuniacha, afu ukimbilie wapi? Mmmmmh! Ondoa hayo mawazo. Bibie V akanyweaaaaaaaaaa!

Haya ndo maneno sio mtu anakupotezeamda afu anakwambia BYE kijingajinga unakubali tu. Thubutuuuuuuuuuuu!
 
Ila happ hata akiolewa ni majanga, jamaq ni tegemezi

Sio tegemezi ni MVIVUUU. Akiamua akaanda event anapataga 5m kwenda juu. Sema sasa uvivu mpaka kodi iwakae kooni ndo afanye manuva yake ya event. Alipataga Tangazo moja la maana, akalipwa hela ndefu wacha amnunulie bibie bonge ya usafiri.
 
Aseeee mjini apa jamaa anahudumiwa na mwanamke, hana maarifa na umri unaenda = catastrophe
 
Back
Top Bottom