Lazima Turekebishe Makosa Haya Kwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lazima Turekebishe Makosa Haya Kwanza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SolarPower, Jul 4, 2011.

 1. S

  SolarPower JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 226
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Toka tupate Uhuru nchi yetu imekuwa ikitumia fedha nyingi sana kwa ajili ya ujenzi wa barabara za lami hapa nchini. Bahati mbaya mpaka sasa idadi ya kilomita za barabara za lami hazifiki km 10,000 kati ya zaidi ya km 85,000 za barabara zilizopo nchini ukiacha zaidi ya km 30,000 zilizo chini ya TANAPA. Pamoja na umuhimu wa barabara za lami katika maendeleo, naomba nipendekeze mkakati tofauti ambao unaweza kutusaidia sana katika kutuletea maendeleo kwa haraka zaidi na kupunguza umaskini wa kipato kwa kiwango kikubwa kila mwaka katika nchi yetu.

  MKAKATI UNAOPENDEKEZWA

  Kutokana na takwimu za TANROADS na Wizara ya Ujenzi, gharama za kujenga kilomita moja ya barabara ya lami ni zaidi ya shilingi bilioni moja na milioni mia mbili mpaka shilingi bilioni moja na milioni mia tano. Kwa maana hiyo, OPPORTUNITY COST ya kilomita moja ya barabara ya lami ni kati ya matrekta 50 mpaka 63 yote yakiwa na vifaa vyake muhimu. Matrekta ninayoyazungumzia hapa ni yale yanayouzwa na SUMA JKT pale Mwenge.

  Pendekezo hapa ni kuwa badala ya kujenga say km 350 ya barabara za lami kwa mwaka mmoja, ili kuzifanya zipitike kwa angalau miaka mitano mfululizo na bila tatizo, tutenge angalau shilingi milioni 250 kwa kila kilomita na kuzijenga kwa kiwango cha changarawe ili ziweze kupitika bila tatizo kwa mwaka mzima. Hili likifanyika badala ya kutumia zaidi ya shilingi bilioni 420 mpaka shilingi bilioni 525 kujenga km 350 tu za barabara ya lami, tutaweza kutumia shilingi bilioni 17.5 kila mwaka na kuhakikisha kuwa hizo km 350 zinapitika kila mwaka bila tatizo lolote wakati huo huo tukiokoa zaidi ya shilingi bilioni 332.5 mpaka shilingi bilioni 437.5 kwa hiyo miaka mitano. Iwapo fedha hizi zikitumika kununua hayo matrekta tuna uhakika kama taifa kupata zaidi ya matrekta 13,854 mpaka matrekta 18229. Kwa idadi hii ya matrekta kila mwaka tutakuwa na uhakika wa kulima kwa njia ya kisasa zaidi zaidi ya ekari milioni 15. Kwa makisio ya chini kabisa ya faida ya ekari moja ya shilingi laki moja, kila mwaka kama taifa tutapata zaidi ya shilingi bilioni 1,500 kama faida kwa kutumia mkakati huu na kiwango hicho kilichopendekezwa lakini wakati huohuo hizo kilomita 350 za barabara zikipitika muda wote wa mwaka bila tatizo lolote. Kwa faida ya zaidi ya shilingi bilioni 1,500 tutakuwa na uhakika wa kuwa na zaidi ya km 100,000 za barabara ambazo zitakuwa zinapitika kila mwaka bila tatizo lolote lile. Katika hili naomba tujifunze toka kanda ya Ziwa kwa barabara zilizojengwa kwa gharama ya UNCDF na UNDP miaka ya 2000 mwanzoni. Kwa maneno mengine tutaweza kujenga zaidi ya KM 1000 za barabara za lami.

  "KINACHOTAKIWA KWANZA NI UHAKIKA WA BARABARA ZETU KUPITIKA MUDA WOTE WA MWAKA. BAADA YA KUWA NA UHAKIKA KUWA KILA MWAKA BARABARA ZETU ZOTE ZINAPITIKA BILA TATIZO NDIYO SASA NGUVU ZAIDI ZIELEKEZWE KWENYE UJENZI WA BARABARA ZA LAMI."

   
 2. S

  SolarPower JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 226
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama alivyosema Waziri Mkuu wa zamani wa India "KILA KITU KINGINE KINAWEZA KUSUBIRI, LAKINI SI KILIMO". Ni muhimu sana tukatekeleza falsafa hii kwa vitendo kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu na watu wake.
   
Loading...