Actually , this is a very pressing matter all over the world!
Imani hizo zipo na nina imani wengi wetu (hapa JF) tuna mawazo hayo na tunaamini kabisa kwamba tukipelekwa kuzikwa kwetu tunaungana na ndugu zetu waliozikwa tangu kale!..Kwa makabila makubwa kama Wahaya,Wachaga na Wanyakyusa, mtu hazikwi mbali na kwao, regardless ya umbali wa mtu huyo anapofia!
Ni wachache sana (kama wapo)wanaokumbuka kufacilitate ishu ya kuufikisha mwili wake makwao pindi atakapokufa!...
Kama mtu alikuwa na uwezo, basi kiasi cha mali zake kinaweza kusaidia hilo, lakini, asilimia 95 huwa ni kushikana mashati na kukamuana kama ulivyosema...Angalau kama marehemu alikuwa mtumishi wa mahali fulani inasaidia, maana mara nyingi organisation zinakuwa na sera ya kumrudisha mtu 'place of Domicile.
Kuna mtu kijijini kwangu alichonga sanduku ambalo alidai azikwe humo pindi akifa, watu walimwona kama mchuro, wazee wakamwita ajibu shauri hilo, na hatimaye sanduku hilo lilivunjwavunjwa![/COLOR]