Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Ndiyo maana sisi wengine ambao tunaiona hii serikali ni Imara tunaihamasisha wampeleke Lowassa kwenye Mahakama ya Ufisadi, kinyume cha hapo wakae kimya!!

unataka wakae kimya mara ngapi?! toka 2008 hadi sasa bado unategemea kuna jipya?! we endelea kuiona imara
 
Imagine unampeleka Lowassa Mahakamani halafu anapata Mawakili huku Lissu kule Kibatala
Kwangu mimi mawakili siyo hoja, hoja hapa ni kwa nini kila siku watu wanatulazimisha tuamini kwamba Lowassa ni Ufisadi na Ufisadi ni Lowassa. tunataka tufikie mwisho!!
 
Kwa hiyo Magufuli ni Raisi wa Tanganyika sio ?? Kwa sababu Zanzibar wana rais wao ?
Tofauti yake ni kwamba Rais wa Jamhuri anapigiwa kura mpaka Zanzibar lakini waziri Mkuu ni msimamizi wa mambo ya Tanganyika katika Muungano. Wanaodhulumiwa ni Wazanzibari!!
 
Tofauti yake ni kwamba Rais wa Jamhuri anapigiwa kura mpaka Zanzibar lakini waziri Mkuu ni msimamizi wa mambo ya Tanganyika katika Muungano. Wanaodhulumiwa ni Wazanzibari!!
Mbona tunapenda kupotoshana sana ? Kila kitu ni siasa tu ,Waziri Mkuu yeyote yule ni waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania hayo mengine mimi siyajui ,mpaka Zanzibar itakapoamua kujitoa kwenye Muungano
 
Mzee hiyo Richmond ni chain utashangaa hata usiowafikiria nao wamo !! Ww acha yaishie hapo hapo tuanze upya hakuna alie msafi utawahukumu wengi tu acha ubishi uende mbinguni
 
*****
GO TO COURT.....
for lowassa issue/
HII YA ESROW NA LUGUMI NA MEREMETA PIA ZIPO HOT KWELI...
..HILI HILI LA M/V DAR ES SALAAM SI LA KUFUMBIA MACHO
 
Huyu si mfuasi wa magufuli mleta mada nashangaa kapata wapi courage ya kumtaja
 
Mbona tunapenda kupotoshana sana ? Kila kitu ni siasa tu ,Waziri Mkuu yeyote yule ni waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania hayo mengine mimi siyajui ,mpaka Zanzibar itakapoamua kujitoa kwenye Muungano
anakuwaje wa Muungano kama hana mamlaka wala madaraka Zanzibar? Inapotajwa Tanzania si lazima ihusishe na Zanzibar. Wenzetu wa Zanzibar ndiyo wanaodhulumiwa!!
 
Richmond ni ya kikwete
 
Pole sana kwa kujitafutia matatizo maana naona unawatafuta serikali kwa kuwaona hawajui wajibu wao jiangaie
 
anakuwaje wa Muungano kama hana mamlaka wala madaraka Zanzibar? Inapotajwa Tanzania si lazima ihusishe na Zanzibar. Wenzetu wa Zanzibar ndiyo wanaodhulumiwa!!
Huwezi kuniambia inapotajwa Tanzania sio lazima ihusishe Zanzibar ,kwani Tanzania ilipatikanaje ?? Tanganyika+ Unguja + Pemba=Tanzania

Hilo la kudhulumiwa ni swala lingine kabisa anzisha thread yake

Wewe una uhakika gani Waziri mkuu hana mamlaka na mambo ya Zanzibar ? Wanapokula viapo vya kutotoa siri wewe unafikiri ni siri zipi hizo ??
 
Mwadilifu alificha ukweli tangu 2008 leo anajigamba kwamba kwa ushahidi alionao hakuna wa kusalimika.? eti alipiga magoti kuomba kwa mungu...halafu akaficha ukweli !inashangaza ! any way nasikia shetani ndio baba wa uongo na yawezekana maombi yao yalitekwa na kujibiwa na shetani-baba wa uongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…