Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Acha atutembeze katika barabara ya ukweli
Hawezi kufungwa tupo tutamdhamini.

Ukweli Upo na umekuwa ukiishi katika fikra zetu.
Ukitaka asisemwe Basi aachie ofisi ya umma.

Alipo sasa yeye ni waumma.
Lazima asemwe.
Bora ukachunge ng'ombe kuliko kudharau Mamlaka. Utaishia jela bure!
 
Acha ujinga wewe, nenda mahakamani haraka sana acha kutafuta kick. Alafu we mwandishi kwa kukushauli tu, rudi shule ukatoe ujinga kwani elimu bure saizi.
 
Acha ujinga wewe, nenda mahakamani haraka sana acha kutafuta kick. Alafu we mwandishi kwa kukushauli tu, rudi shule ukatoe ujinga kwani elimu bure saizi.
Umekuwa mjinga kama jina lako "APUTWIKE". Endelea na ujinga wako!!
 
ukiyaleta ya Lowasa ni sawa na kuyaleta ya nyumba za serikali,kivuko cha bagamoyo,Escrow na mengine mengi.kumshtaki Lowasa ni sawa na kuishitaki serikali iliyopo madarakani
 
Kwa nini sasa wanaendelea kumsakama?
Hoja kama hizi zinakupunguzia sifa japo unajiona kama unaonekana jasiri na mabavicha wenzako
Mahakamani si pa kumuombea mtu kupelekwa awe na ushahidi au la,lakini kwa akili za Bavicha hili unalitaka
Na subiri litakuwa soon,na akifungwa mtu wako usije kusema mahakama imenunuliwa
 
Magu mwenyewe anasema anadili na ufisadi wa miaka mitano iliyopita, je ndani ya hiyo miaka Lowasa alihusika na nini?

Kama kuna ushahidi kesi jinai haina mipaka ya muda (limitation of time). Hata EPA inaweza kuletwa. Wanaharakati mmelala?
 
Mweeeeeeee!

Unataka wajitumbue wenyewe siyo???

Kwani hukumsikia mwenyewe anasema kuwa "Ni lipi alilolifanya Mweshimiwa Raisi hakulijua???"

Mi naomba walipotezee tu maana hata ubora na viwango vya Anko Magu hatutaviona tena. Na kwa hakika ni heri wakaruhusu mikutano na maandamano kuliko kufungulia hiyo kesi.

Wangu mtizamo tu huo lakini....!
 
Kama ingekuwa hahusiki kwa nini ajiuzulu? Mbona Pinda kuna wakati alipewa shinikizo lakini hakujiuzulu? Alikimbilia "UWAZIRI MKUU" kama namna ya kufuta aibu ionekane ameonewa. Asingeweza kuacha UWAZIRI MKUU bila sababu ya msingi. Halafu huyo wa juu aliyemuagiza mbona hamsemi? Acheni mahaba, HANSARD iko wazi inaeleza RICHMOND SAGA kwa mapana yake!
 
Gangongine huu mchezo hauhitaji hasira.Kwenye hotuba hiyo ya Lowassa kuna maswali yanahitaji majibu lakini mpaka sasa hamtaki kutujibu.

  1. Spika alipewa ushahidi na Lowassa ili ampe Mwakyembe na Mwakyembe alipewa huo ushahidi lakini hakuutumia. Kwa nini?
  2. Kina Mwakyembe walisafiri hadi Marekani kuhoji mashahidi lakini hawakumhoji mtuhumiwa aliyekuwa na ofisi yake mita 200 toka Ofisi za bunge. Kwa nini?
  3. Sakata la Richmond mpaka Lowassa anajiuzulu taifa lilikuwa limepata hasara kiasi gani? Kwa nini haisemwi ni hasara kiasi gani imepatikana?
  1. Mitambo ile iliyoletwa na Richmond ndiyo hiyo hiyo iliuzwa kwa Dowans kisha Dowans wakaiuza kwa Symbion ambao nao wanaitumia kuzalisha umeme wanaouziwa Tanesco. Uharamu wa Richmond ulikuwa ni mitambo au ulikuwa nini hasa?
 
Afadhali sasa mahakama ya mafisadi imeshaanza kufanya kazi. Ila nimesikitika sana mtu wa kwanza kushitakiwa siyo Lowassa.
 
Afadhali sasa mahakama ya mafisadi imeshaanza kufanya kazi. Ila nimesikitika sana mtu wa kwanza kushitakiwa siyo Lowassa.

Kikwete aliwackear wote Chenge na Lowassa, akasema hakuna pesa zilizopotea. Huwezi kumushitaki Lowassa bila ya Kikwete. Kikwazo kipo hapo.
 
Kikwete aliwackear wote Chenge na Lowassa, akasema hakuna pesa zilizopotea. Huwezi kumushitaki Lowassa bila ya Kikwete. Kikwazo kipo hapo.
Nimeamini maneno yako maana leo Gazeti la chama chao limeandika kwamba mahakama ya mafisadi imekosa kesi. Inakosaje kesi wakati walituambia hiyo mahakama ya Mafisadi ikianza Lowassa atakiona cha mtema kuni!
 
Kama wana kesi na Ushahidi wa kutosha, Wangesubiri nini hadi leo kumkamata na Kumshitaki? Hamtumii akili zenu? Lowassa ameshaingia Upinzani kwahyo serikali hawana sababu yoyote ya kumlinda kwa sababu sio mwenzao tena, Kwanini Wamemuacha? Unazan wanamwogopa?Kwa lipi?? Fikiri kabla ya kupost, Nyambaf
 
Huyu si ndio waziri wa sheria aliyesimamia uanzishwaji wa mahakama ya mafisadi ?

Mkuu Mwakyembe nakung'ata sikio , usipompeleka lowassa mahakamani iko siku utapelekwa wewe kwa upotoshaji wako , abhajanga abho abikusyobha , Lwako gwimwene nu bhutunghulu bwako .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…