Lazaro Nyalandu: Hakuna Chama cha Siasa kinachoweza kutawala milele

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Hakuna Chama cha Siasa kinachoweza kutawala milele. Tutunge sheria kulinda haki na uhuru wa Vyama vya Siasa kujiendesha kwa dhamana na utashi wa wanachama wao. Nawasihi sana WABUNGE na SERIKALI kuutazama upya MUSWADA wa SHERIA ya Vyama Vya Siasa. USIPITISHWE kuwa sheria. HAUFAI.
 
Alichosema Nyalandu ni kweli na hiyo ni kwa sababu yuko upinzani, angekuwa ccm angeunga mkono hiyo sheria, na hata sasa akirudi ccm usishangae akapatiwa kipindi maalum kuelezea hiyo sheria ilivyo nzuri.
 
Muswaada una kila dalili ya kupitishwa na kina Iyena iyena.
La muhimu upinzani ujiandae na plan B.
 
Alichosema Nyalandu ni kweli na hiyo ni kwa sababu yuko upinzani, angekuwa ccm angeunga mkono hiyo sheria, na hata sasa akirudi ccm usishangae akapatiwa kipindi maalum kuelezea hiyo sheria ilivyo nzuri.

Huenda!ila Nyalandu hapelekeshwi hovyo hovyo aisee
 
Hakuna Chama cha Siasa kinachoweza kutawala milele. Tutunge sheria kulinda haki na uhuru wa Vyama vya Siasa kujiendesha kwa dhamana na utashi wa wanachama wao. Nawasihi sana WABUNGE na SERIKALI kuutazama upya MUSWADA wa SHERIA ya Vyama Vya Siasa. USIPITISHWE kuwa sheria. HAUFAI.
Ni kweli milele sio mchezo. Ila chama cha siasa kinaweza kutawala miaka mingi hadi kuwavusha watu kutoka hatua moja ya maendeleo hadi nyingine. Ona china cuba na vietnam wanaendelea ila nchi nyingi kama haiti na barani afrika vyama vingi vinatumika na nchi zenye nguvu kuwagawa watu kwa maslahi yao.
 
Hahaha na hakuna dalili za ccm kuondoka wala kufa, wanatujaza upepo tu hawa.
 
Ni kweli milele sio mchezo. Ila chama cha siasa kinaweza kutawala miaka mingi hadi kuwavusha watu kutoka hatua moja ya maendeleo hadi nyingine. Ona china cuba na vietnam wanaendelea ila nchi nyingi kama haiti na barani afrika vyama vingi vinatumika na nchi zenye nguvu kuwagawa watu kwa maslahi yao.

Acha utoto ww, siku ile tumeona mabox ya kura yakitolewa ndani ya vituo vya kura na kwenda kujazwa kura za ccm ni hayo mataifa yenye nguvu yaliagiza? Uchu wa madaraka wa viongozi wetu ndio tatizo. Hakuna cha mzungu wala nini.
 
Back
Top Bottom