Laurent Gbagbo yuko kwenye jengo lililopo nyuma ya geti hili chini ya ulinzi (kama alivyosema Jasusi), kwenye mji wa Korhogo uliopo kaskazini mwa Ivory Coast, akingojea kesi yake.
Hali yake sio mbaya (Gbagbo bado anakula bata)!
Huyu ndie mwendesha mashtaka Simplice Kouadio Koffi (kushoto) akiwa pamoja na kamanda Fofie Kouakou wa kanda ya Korhogo walipokuwa kwenye nyumba ya Gbagbo. Mahojiano na Gbagbo kuhusu kesi yake yameanza Jumamosi iliyopita. Ingawa wanasheria wake (Gbagbo) hawakuhudhuria mahojiano hayo daktari wake wa binafsi alikuwepo.
Kuna tofauti kati ya Gbagbo na Balali (bilali?). Gbagbo anajulikana alipo na ameshatembelewa na Bishop Desmond Tutu, Kofi Annan, na Mary Robinson (UN Human Rights chief)