GE2025 Larry Madowo: Sijaenda kuripoti Uchaguzi wa Tanzania kwani inahitaji kibali ambacho hawatoi. Tunajua kinachotokea ikiwa Serikali haikupendi

GE2025 Larry Madowo: Sijaenda kuripoti Uchaguzi wa Tanzania kwani inahitaji kibali ambacho hawatoi. Tunajua kinachotokea ikiwa Serikali haikupendi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,559
Reaction score
3,953
Mwandishi wa habari wa Kenya anayefanya kazi na CNN, Larry Madowo, ameweka wazi sababu za kushindwa kuripoti kuhusu uchaguzi mkuu na maandamano yanayoendelea nchini Tanzania dhidi ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza siku ya Alhamisi, Larry alisema kuwa Serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya iwe vigumu kwa waandishi wa habari wa kigeni kufanya kazi kwa uhuru nchini humo.



"Tanzania haitaki uandishi huru unaokosoa. lli kufanya kazi nchini humo kama mwandishi wa kigeni, nahitaji kibali maalum cha serikali (media accreditation). Kihistoria, Tanzania haijawahi kutoa vibali hivi kwa urahisi. Ilikuwa changamoto hata enzi za Rais Magufuli, na hali haijabadilika chini ya Rais Suluhu," alisema Larry.

"Naweza kwenda kama mtalii, lakini si kuripoti. Na tunajua Tanzania inavyowachukulia wale ambao haiwapendi," aliongeza.


Kauli yake imekuja wakati ambapo maandamano na mvutano mkubwa unaendelea nchini Tanzania kufuatia uchaguzi mkuu wa Jumatano, ambao wakosoaji wameuita "uchaguzi wa maigizo" na "ushindani wa pande moja" baada ya wagombea wakuu wa upinzani kuzuiwa kushiriki.

Kwa sasa, vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa haviripoti moja kwa moja kutoka nchini humo, jambo linaloongeza hofu kuhusu uhuru wa vyombo vya habari na udhibiti wa taarifa na serikali.
 
Back
Top Bottom