Laptop yangu aina ya Dell Latitude D420 haiwaki,

wete

Member
Nov 16, 2012
66
125
Heshima kwenu wakuu

Laptop yangu aina ya Dell Latitude D420 haiwaki, nikiiwasha inaishia kuwasha ivi vitaa vya caps lock, Bluetooth na vinaonesha mwanga kwa sekunde kadhaa alafu vinazima na ndo inaishia hapo hapo bila kuonesha chochote kwene display, nimechomeka power pia taa ya battery inaindikate kama inacharge sasa hapa nashindwa pa kuanzia ndo sababu nikaonelea niliweke hapa wakuu kwa msaada wenu tafadhali
 

MANDELAA KIWELU

JF-Expert Member
May 16, 2011
3,735
2,000
Tatizo litakuwa ni hapo kwenye nyaya za mwanga .. Ili kujiridhisha tafuta desktop screen na uunganishe na hiyo laptop yako uangalie kama itafanya kazi kwenye hiyo desktop screen.
 

Msafiri Kasian

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,004
1,500
Nadhani ungeanza kwa kueleza hilo tatizo lilianzaje? Na je vipi unapoiwasha, inazima baada ya kuonyesha chochote kwenye screen?

Kama hakuna chochote kinachoonekana kwenye screen pengine kuna tatizo na display kwenye sreen na sio operating system (windows). Embu jaribu kutoa battery na connect moja kwa moja adopter alafu uwashe.
 

Cham Bee

JF-Expert Member
Feb 10, 2015
3,490
2,000
Chukua monitor/kioo cha kawaida ili uweze kuhakikisha kama itawaka basis tatizo litkuwa ni kioo.Endapo haitawaka fungua sehemu ya ram kisha safisha sehemu hizo pamoja na ram yenyewe kwa mswaki au brash yoyote kisha rudishia.Kama haitakubali kuwaka tatizo litakuwa ni Graphic ambayo huwa ina kawaida ya kuregea kutokana na joto jingi so ni lazima mashine ifunguliwe then graphic ipashwe moto kwa kutumia kifaa maalumu.Kuna wakati inaweza kuwaka kisha ikagoma.
 

moe junior

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
800
1,000
Ikishindikana kuwaka, me nna d410 imepasuka kioo... Utaniuzia kioo na hdd
@kufakufaana
 

wete

Member
Nov 16, 2012
66
125
Chukua monitor/kioo cha kawaida ili uweze kuhakikisha kama itawaka basis tatizo litkuwa ni kioo.Endapo haitawaka fungua sehemu ya ram kisha safisha sehemu hizo pamoja na ram yenyewe kwa mswaki au brash yoyote kisha rudishia.Kama haitakubali kuwaka tatizo litakuwa ni Graphic ambayo huwa ina kawaida ya kuregea kutokana na joto jingi so ni lazima mashine ifunguliwe then graphic ipashwe moto kwa kutumia kifaa maalumu.Kuna wakati inaweza kuwaka kisha ikagoma.
Inawaka kwa sekunde kama 6 hivi afu inapoteza moto kabisa, na pia haidisplay na nikiskiliza feni yake siskii chochote ila charge inapeleka kama kawaida mkuu
 

JaffarMohammed

JF-Expert Member
Nov 13, 2016
764
500
Kwanza kabisa nadhani ni vyema ungekubali kugawa riziki ili na waliosomea ama wanaojishugulisha na kazi hizo waweze kulisha familia zao ambazo zinawategemea. Maana tunapokwenda watu watauliza hata jinsi gani wafanye operation za ubongo humu JF.

Baada ya kuandika hayo
yafuatayo ni ya kuzingatia kama walivyotangulia kukushauri.

1. Kama ukiwasha laptop yako ukaona maneno fulani yanaonekana kwenye screen ujue screen yako ni nzima kabisa ila kuna tatizo la boot device ama operating system. Ukiona haiandiki kabisa wala huoni maneno yoyote then angalia point namba mbili

2.Kuna keys fulani kwenye keyboard ambazo hua zikibonyezwa kwa pamoja zina switch kati ya screen ya laptop kwenda kwenye screen ya pembeni. Hii ni kukiwezesha kuendelea kuyumia CPU yako hata kama screen ya laptop imeungua. Kuna uwezekanao zilibonywezwa keys hizi.

3. Kama unaweza kupata screen ya pembeni hata kwa jirani ni vyema ukajaribu kuunganisha kwenye laptop yako ili uweze kuona kama itaonesha.

4. Ukiona yote hayo yameshindikana hebu kubali kugawa rizki mafundi wapate kulisha familia zao kama nilivyokwisha kuandika.
 

Adolf Hitler Jr

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
344
250
Kawaida kwa wenye uzoefu na laptop za Dell ni tatizo la kawaida, hold the power button for almost 20 seconds then itawaka.
 

mwenyewe joseph

Senior Member
Nov 1, 2016
104
225
Hii!!
Jaman hata mmi Nina lenovo yangu tatizo ni hilohilo inawaka vitaa vya kuonyesha kama inapeleka charge tu haidisplay mwenye screen

Msaada ndugu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom