laptop zipo za aina nyingi, na hakuna laptop ambayo inakidhi mahitaji yote, ikiwa na nguvu sana haitakaa na chaji, na ikikaa na chaji sana nguvu itakuwa ndogo. na laptop nzuri zinaenda milioni 4 mpaka 10 zikiwa na specification za kisasa.
hivyo ni vyema kutambua matumizi yako ili upate kifaa kizuri kwa ajili yako.
kwa around dola 700 mpaka 800 ndio unapata laptop nzuri zinazotick matumizi mengi laptop kama
-dell xps 13
-asus zenbook ux305
-lenovo yoga series
-hp envy series etc
hizo hapo juu utakuta ram kama 8gb, ssd kama 256Gb na processor za core m, i5 au i7
kwenye biashara nako kuna laptop zake, wa video editing wana laptop zao etc