Kweli nimeamini sikio la kufa halisikii dawa. Yaani pamoja na ukweli kwamba Magamba wameshikwa vibaya Arumeru bado wanajidanganya kuwa watashinda uchaguzi mdogo.
Mleta hoja anadai mkutano umejaa watu wakati mie niko hapa uwanjani watu waliokuwepo kabla msafara wa mkapa haujafika walikuwa wakihesabika. Wameongezeka baada ya mzee Mkapa kuwasili na msafara wa magari zaidi ya 50 uliojaa watu kutoka Arusha mjini, Monduli, Moshi na Babati ambao wengi wao siyo wapiga kura Meru.
Kama kweli wamejaa weka picha kuthibitisha na ukidanganya naweka picha inayoonyesha ukweli.