Radhia Sweety
JF-Expert Member
- Aug 10, 2011
- 4,433
- 1,772
Kwa asilimia kubwa, nchi za dunia ya tatu zinaendesha bajeti zao kwa kutegemea misaada kutoka nchi zilizoendelea, hususani Marekani na Jumuiya ya Ulaya.
Watoa misaada hao wamekuwa wakitumia udhaifu huo wa umaskini kutengeneza urafiki wa kinafiki na vyama vya siasa vinavyoongoza nchi hizi fukara.
Tanzania ni miongoni mwa nchi hizo. Tangu uhuru imekuwa ikiishi kwa misaada ya nchi za magharibi na kwa vyovyote vile nchi hizi ni wanufaika wakubwa wa rasilimali zetu. Na kwa vyovyote vile CCM imeshajitengenezea urafiki mkubwa na nchi hizi.
Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi, ushindani mkubwa ukiwa baina ya mgombea wa CCM(John Magufuli)na yule wa Ukawa(Edward Lowassa). Hisia nyingi mtaani ni mapenzi makubwa kwa mgombea wa Ukawa.
Lakini wazungu wanamkubali Lowassa kiasi hiki kweli? Wazungu wapo tayari kuona mabadiliko kweli?Kuna sababu gani za msingi zitakazowafanya waiondoe CCM madarakani kama zipo?