Lakini Polisi wa Tanzania ni Typical. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lakini Polisi wa Tanzania ni Typical.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lekanjobe Kubinika, Jan 14, 2011.

 1. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nadhani mafunzo yao ya upolisi kipaumbele chake vurugu tu na sio kufuata utaratibu wa kujali raia. Nchi zingine Polisi unaweza kumtegemea kabisa akuongoze uwe salama hata kama ni mgeni kabisa. Watakuuliza na kujadiliana nawe na hata kukupatia maamuzi mbadala na kwa faida na hasara, watakushauri wanayodhani ni salama zaidi kwa uzoefu wao. Polisi hutegemewa sana na ni rafiki wa raia mwema.

  Polisi Tanzania hawajui upole kama msamiati wenye tija katika kazi zao. Angalia hata kwenye makambi yao kuuana wenyewe kwa wenyewe kila mwaka kunavyoripotiwa, tena kwa sababu za kijinga kweli kweli - ati wameporana wanawake ambao wala sio wake zao bali mahawara tu.

  Hata kabla ya Arusha hajaisha wakingali wanatafuta sababu kujihalalishia mauaji ya raia wasio na silaha, kule Mbeya nako wameshaua. Zamani nilifundishwa nikiwa JKT kwamba polisi anafundishwa kuvunja miguu ya mtuhumiwa anayetaka kukimbia ili aisaidie polisi, lakini leo wanajifunza kutoboa mioyo vifuani kwa raia? Tangu Mkapa alipowapandisha vyeo mapolisi walioua raia Zanzibar kwa sababu za kisiasa, wimbi la kuua raia linapamba moto. Yaelekea ukiua ni sifa moja nzuri sana kwa mapolisi nkupanda cheo haraka. Wewe ua halafu sema alikuwa jambazi sugu, cheo hichoooo?

  Inatia kichefuchefu polisi na serikali kutetea kuua raia wema kwa kisingizio chochote kile wakati wa amani. Sidhani kwa kufanya hivyo kunahamasisha raia wawe wema kusaidia polisi kudhibiti uhalifu, maana mauaji na jeuri zao zinawazuia raia wasiwapekee taarifa muhimu.

  Pale Tegeta tarehe 31 Desemba 2010 nilipokuwa napita pale, nilimwona traffic amepanda kwenye lori lililopack pembeni, kisha akawa anazuia magari yaliyoko kwenye foleni komavu pale darajani ili aingie kwenye msafara wakipelekana kituo kidogo cha polisi pale Tegeta. Ghafla walipofika CCM wakaanza kubishana na kuanza kung'ang'aniana usukani na dereva wa lori hilo. Baadaye lori likachochewa mafuta na kuparamia pikipiki na gari zilizokuwa mbali kabisa na barabara. Kisha wananchi walipoona wakapandisha hasira na kuanza kumtwanga traffic ambaye alikimbilia gaari nissan iliokuwa njiani kwenda Kibaoni huku akifukuzwa na raia wenye hasira.

  Nilijifunza kwamba raia wanajua udhaifu wa polisi na kubwa ni rushwa. Huenda dereva aliambiwa atachomekewa kesi asipotoa kidogodogo, ndipo purukushani zikaanza. SIjui kama walipona watu, maana sisikii tena. Hao ndio mapolisi wetu Bongo. Ukienda Kituoni wakakuweka ndani usidhani nutatoka for free. Wana kiwango kabisa bila risiti, tena lazima wakubwa zao wawagawie mafungu, maana hujitetea kwamba hawapunguzi kwa vile bosi hataelewa.
   
Loading...