Lakini Mbowe unatukosea

Lakini Mbowe unatukosea

TAMKO

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2011
Posts
1,090
Reaction score
763
Mzee Unatukosea, Unatunyima Raha ya Siasa Ndani ya Nchi hii. HASIRA, VISASI NA CHUKI Havijengi chair wetu.

Kuna MATUKIO najaribu Kuunganisha Dots kupata Sentensi Kamili. Na Picha Inaanza Kuja, I am sorry Dears MBOWE ANATUMIKA KUUA CHAMA.

Why

1: Chama Ni Cha Kidemokrasia Lakini hakiendeshwi kidemokrasia mfano maamuzi ya kutoka Bungeni talifanya na watu Wanne kwenye tu.

2: Chama Sio Cha wabunge CHAMA NI CHA WANACHAMA, Lakini maamuzi Makubwa kabisa ya HATARI SANA yanafanywa na Kikao Cha watu wachache ambao ELIMU na TAALUMA ya Kile wanacho kiamua HAWANA..

3: Wanatolea Maamuzi kwenye Mambo yanayo hitaji Tafiti Makini Lakini Kwa Kukurupuka au bendera Fuata Upepo wanataka Chama Kiendeshwe Hivyo.. Baada ya Corona Kuingia Nchini Marekani, Kabla ya Kufanya Lockdown, Walitathimini Kwa Karibu Madhara ya Lockdown na wakatathimini Madhara ya kutofanya Lockdown pia. tafiti walizo Pata zikajadiliwa Kwa kina. Kwamba Iwapo Marekani itafunga INJINI YAKE YA UCHUMI (Economic Machinery) die to Lockdown, Kwa Wiki mbili Hadi Tatu, kisha baada ya Hapo wakaufungulia Uchumi tena, Mwisho wa Mwaka wakifanya mahesabu ya Uchumi kwenye Jumla ya Matumizi (Expenditure approach) na Mapato(income approach) uchumi utayumba Kwa 18-22%. Wakatadhimini Madhara yake na Maisha ya wananchi wake.

Marekani wakaamua kuhatarisha Uchumi wao ili kunusuru maisha ya Mwananchi wake Kwa Wiki mbili Hadi Tatu. Majimbo mengi marekani walianza stay- at-home Orders, Kuanzaia March 20. Na wengi walipanga Hadi Mwezi wa Nne Reatrictions iishe. Lakini Hali ndio ikawa Mbaya zaidi. the Pandemic imepiga vibaya na Kuua wengi sana .hadi Kufikia THIS MAY 20 Watatumiza Miezi Miwili average..! Kama Kwa wiki mbili tatu uchumi ungeyumba Kwa robo sasa Kwa miezi miwili Hali Itakuwa Mbaya Mno, this Demage will cause Economic instability Kwa Miongo kadhaa ijayo.. sawa Wanaifungua MAREKANI TENA despite kwamba The Pandemic ndio iko kwenye kasi.. wonderfull. Nchi Za Ulaya zima miezi zaidi ya Miwili ya lockdown.

Lakini Mbali na Hapo, Itawachukua Muda mtefu tena kujenga Uchumi wao Lakini watakuja ujenga tu kwa Sababu wanazo malighafi za Kukuza Uchumi Tofauti na Nchi zetu Za Kiafrika ambao maskini Hatuna malighafi Za Kujenga Uchumi , Uchumi ukipiga mweleka ni Kulala Hapo Hapo..mnakumbuka Vita Ya Iddi amini 89/79 tokea Uvamizi wa Mzee Iddi Hadi Kutolewa Nje ya Mipaka Yetu na Kisha kutolewa Njia ya Uganda na obote kurudishwa na Kupewa Ugali wake ilichukua miezi Nane. Lakini Uchumi wetu Uliporomoka mpaka Leo hii! Sidhani kama historia Hizi ni Ngeni Lakini Kwa Makusudi watu wanaamua kwenda kinyume nazo..

4: Mzee Mbowe na Wabunge wetu Mmejisahau, Mmesahau Dhima ya Uwakilishi. UKIWA MBUNGE Wewe ni Mwakilishi, Wewe ni Sauti ya Watu sio Sauti ya Mtu. Kikundi kidogo mnapo kaa na Kufanya maamuzi HATARI, Ya kuwakataza wajumbe kuwakilisha watu wao kwani Nyie ndio MLIWACHAGUA? Wajumbe walichaguliwa na Wananchi waacheni wananchi waamue juu ya wajumbe wao sio Chama.

5: Kwa Makusudi Mbowe Anatengeneza Kisirani kati ya Chama na wananchi. Ni kujisahau sana kutojua MIPAKA YA CHAMA NA MIPAKA YA UWAKILISHI. Kumwondolea Mbunge Sifa Za Kuwa Manachama means Kumfuta Chama Ni kuwanyanyapaa wananchi walio mchagua, na kuwakasirisha Wananchi Dhidi ya Chama . Ni SIASA Gani MWENYEKITI ANAIJENGA?

6: Mwenyekiti na Kundi lako Mnajifanya “MUCH KINOW SANA” mnakosea sana. Chini ya Uongozi wako 2010/15 Chama Kilikuwa “HOT” sio Kwa Sababu ya Uongozi wako Bali Chama Kilikuwa na Washauri wazuri. Chama Kilikuwa kikipiga kinatua kwenye Hitaji halisi la Mwananchi! Na Kila walicho kiongelea kilikuwa wazi na Kweli! Lakini CHADEMA ya 2015 Mbali na Kuwa na Wawakilishi wengi zaidi Lakini IMEFUBAA..

Kufubaa Kwa CHADEMA ni Pale Baada ya Kete zote ambazo walizitumia kuinanga Serikali zilichukuliwa Serikali na Kuanza kutendewa. CHADEMA ikakosa KETE Mkononi, CHADEMA wakashindwa Kubadilika sambamba na Mabadiliko ya siasa na Uongoz, Ingawa mwanzoni kabisa CHADEMA walionekana kukubali Uongozi wa Rais Magufuli hasa baada ya Hotuba Yake Pale Bungeni. Matukio Ya Kuanza Kuporomoka Kwa CHADEMA yalianza pale Walipo pokea Ushauri na Mtu aliye washauri amesha rudi zake CCM, Kwamba CHAMA CHOCHOTE CHA KISIASA AMBACHO KINAUNGA MKONO BIDII ZA SERIKALI ILIYOKO MADARAKANI UJUE HAKINA MPANGO WA KUCHUKUA DOLA Ushauri huu Mbaya Kabisa Kutokea Ndio Ulio wafanya KUANZA SAFARI YA KUPINGA KILA KITU Hata kama ni Cha UKWELI. Lakini CDM wanasahau kwamba ni wananchi Hawa Hawa ambao Jana waliwaambia haya ambao leo wanayapinga. CDM wakajitenga na washauri wote wazuri. KIKABAKIA CHAMA CHA KULANA na UHUNI na Kupachikana Mimba.

Leo wanaendelea mwendelezo wa KUKAZA MOYO NA TIMUA TIMUA, Lakini Wangekuwa wanatumimua Kwa Haki, HAKI INGEBAKI KWAO, Lakini KWA DHAMIRA HII YA KUTIMUA.. mbele Watadumbukia shimoni na Kusingizia Nchi Haina Demokrasia Ndio maana Chama Kimekufa. Zitakuwa kerere Za Chura. Chadema Inahitaji NEW BRAIN.. hizi zilizopo zinafanya Siasa Za ninety nine this is 2020..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lilishakufa hilo li chama mdau, achana nalo. Linaongozwa ili mradi siku ipite.
 
Mataga mnajiuliza huku mnajijibu kwa nini mnateseka na chadema wamewafukuza nynyi mnalia wachukueni hao wabunge kama mnawapenda
 
Katika swala LA kufukuza hawa wabunge chadema nawapa big up sana.Taasisi yeyote lazima iwe Na nidhamu, nje ya hapo Ni kikundi cha wahuni tu.wale wabunge walitenda makosa kuasi misimamo ya chama chao.Hats ingekuwa ccm wangefanyiwà hivohivo
 
Katika akili ndogo tu inakuje chama kinatangaza wabunge wake wajiwekwe lockdown siku 14 na wasiingie bungeni mpaka wapimwe Corona huku wako kila mtu anaonekana yuko na safari zake. Huwezi kusema siingii bungeni naenda lockdown kwa sababu ya Corona halafu ukaonekana unazurusha unataka utuaminishe vipi sisi wengine?

CHADEMA imeshindwa kuja na sera mbadala na siasa ya tofauti kikubwa wanataka Magufuli azungumze wakosoe tu. Wanataka Tanzania iwe kama ndege inaendeshwa na marubani wawili, kitu ambacho hakiwezekani. Kwa sasa wanacheza na nyimbo na mziki unaopigwa na Magu. Kuwa kiongozi bora ni pamoja na kukubali kuwa umeshindwa na mwelekeo m,bovu wa chama unatakiwa uwajibike. Mh Mbowe kama huko humu ndani wajibika na achia madaraka, bila kuwa na upinzani imara nchi yetu itarudi kwenye mfumo wa chama kimoja. Kuna viongozi wapumbavu wanafanya watu wakakosa imani na upinzani wa kwanza Mbowe. .
 
Katika swala LA kufukuza hawa wabunge chadema nawapa big up sana.Taasisi yeyote lazima iwe Na nidhamu, nje ya hapo Ni kikundi cha wahuni tu.wale wabunge walitenda makosa kuasi misimamo ya chama chao.Hats ingekuwa ccm wangefanyiwà hivohivo

Kumhukumu MTU pasipo Kumpa Nafasi ya KIJITETEA?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi siasa za maji taka hizi nazichukia sana, issue ndogo tuu wanashindwa kuelewana, laiti wangejua rasilimari na nguvu tulizo tumia kujenga network na msingi tena kwa kujitolea tuu, daaa alooooo.........,daaaa nachoka kabisaa yaani ukisikia bita vya panzi furaha kwa CCM ndiyo hii
 
Back
Top Bottom