Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,398
- 14,520
Kampuni ya Universal Music Group East Africa imetangaza rasmi ushirikiano wake na Mwimbaji Staa wa muziki wa Afrika Mashariki, Lady Jaydee ambaye anatambulika kama mmoja wa sauti zenye ushawishi mkubwa na za kudumu katika tasnia ya muziki kwenye ukanda huu.
Ushirikiano huu unaakisi imani ya pamoja kuhusu nguvu ya muziki wa Afrika Mashariki na wajibu wa Wasanii wakubwa katika kuhakikisha unaendelea kukua na kufikia hadhira ya kimataifa ambapo hatua hii inaelezwa kuwa ni muhimu katika dhamira ya Universal Music Group East Africa ya kuibua na kukuza sauti bora zaidi za ukanda huu.
Kupitia ushirikiano huu, pande zote mbili zimejipanga kuinua kiwango cha ubunifu wa muziki wa Afrika Mashariki, kupanua wigo wake wa usikivu duniani, na kuimarisha nafasi yake katika jukwaa la kimataifa.
Universal Music Group East Africa imeeleza furaha yake kuhusu kufanya kazi na Wasanii wenye maono, uzoefu na dhamira ya ubora, ikisisitiza kuwa uwepo wa Lady Jaydee katika ushirikiano huu unaonesha heshima kwa historia yake pamoja na msukumo mpya wa kusonga mbele ambapo wanatarajia kujenga juu ya msingi aliouweka na kuelekea mustakabali wenye mafanikio makubwa kupitia malengo ya pamoja.