Lady Jaydee apiga dongo gizani "kichwa kama tofali"

Migomba

JF-Expert Member
Nov 30, 2013
945
1,334
Katika Naamka Concert wakati akiimba wimbo wa "siwema" kuna kale kamstari eti sababu yeye ni mzuri sana siwezi kupata mwingine kama yeye , jide akamalizia kichwa kama tofali! Watu wakalipuka kushangilia hali iliyoashiria dongo limeenda upande wa pili.
 
Ukitaka kujuwa ukweli mpenzi wako anakuonaje au anakuchukuliaje muonekano wako ni punde mnapo kuwa mmegombana mkatawaliwa na hasira hapo sasa utasikia ya moyoni kila litokalo kwenye kinywa ni la ukweli sema halishindwa kukwambia wakati mpo na furaha...

Utasikia muone kwanza mbaya kama nini najuta hata kwanini nilikuwa na wewe, jitu baya jeusi kama mkaa mfupi kama kimba, wakati ndiyo huyo huyo alikuita sweet, my candy, my wife/husband, my chocolate, honey nakupenda you are real beautiful,wow how handsome you are my husband napenda rangi yako , napenda ulivyo mfupi baby una kichwa kizuri mume wangu, mpenzi wangu wewe ni mrembo kuliko wanawake wote duniani kumbe upande wa pili usitake kujuwa subiri hasira zikija kwani wewe mwanamke gani miguu kama upinde, ndiyo mfano wa jide leo kichwa cha aliyekuwa mpenzi Wake kimekuwa tofali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom