Labda waje wazungu watuhesabie kura

Labda waje wazungu watuhesabie kura

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Kwa hali niliyoishuhudia katika chaguzi mbalimbali hapa nchini na 'mshikemshike' wa kuipitisha Rasimu, ni ngumu kuwa na haki katika chaguzi zetu. Wananchi wanachagua,watawala wanateua. Mfumo uliopo katika kuhesabu na kujumlisha kura hauruhusu ushindi wa kirahisi kwa wagombea au jambo linalopigwa na watawala kuibuka kidedea.

Amini nawaambia, hata Rasimu itapitishwa kwa 'kishindo' na wananchi. Na CCM itashinda kwa ushindi wa kimbuga katika uchaguzi wa mwaka huu na mwakani. Mfumo uko imara.Matayarisho kabambe tayari yameshakamilika. Alichofanya jana Sitta si 'incidental'.Ni 'purely planned'. Ndiyo maana hakuwa na shaka wala tashwishwi.

Jueni ya kuwa kwa mfumo uliopo wa upigaji na kuhesabu kura, huyu huwa yule na hapana huwa ndiyo. Labda waje wazungu watuhesabie kura. Amasivyo,wanademokrasia na wanasiasa mjipange!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
tunapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti ................
 
Naona leo umekuwa mpole baada ya malengo yenu ya kukwamisha rasimu kushindikana.
 
days are numbered,
iwe ni leo ama kesho ama siku hiyo, lakini itafika.
hakuna kinachodumu milele...kama jiwe linasogea lilipo basi hata haya yatapita tu.
 
bado nina matumaini katika uhai wangu nitaona siku ambayo demokrasi imekomaa , serikali inabadilika kwa amani na uchaguzi unafanyika kihalali na hilo ndilo linakua lengo kuu la vyama vyote husika kwenye uchaguzi yaana upinzani na tawala wote wanahuzunishwa na kukana yeyote anaejihusisha na vitendo vya kuchafua demokrasi. Kiongozi tawala anakubali matokeo na kumpongeza mpinzani alieshinda na kuahidi kushirikiana kwa maslahi ya nchi - I still have a dream
 
sharti tukinywee kikombe kwanza ili hiyo ndoto itimie
 
Tangu nizaliwe ndiyo nimehakikisha sasa kwamba hakuna lisilowezekana chini ya jua - kupiga kura muhimu kama zile kwa FAX na Email????
 
Mzee tupatupa ninakubaliana na wewe kwa asilimia mia. Alimradi rasimu 'imepita' (kitu walichokuwa wakikipigania kufa na kupona, na hivyo haishangazi kuona hizo ghiliba na aibu tupu - hawana aibu kabisa), basi ninakubaliana na makada ya ccm kuwa ccm itatawala milele unless utokee muujiza. rasimu hii ya ccm ni kujihakikishia kuwa wataendelea kuwachesha wananchi kama pia. ni masikitiko makubwa kwa umma ambao hauana welewa na ninaamini Mungu yuko na watawala na sio watawaliwa.
 
Watanzania tunapaswa kuwa makini sana katika nyakati kama hizi, busara zinahitajika sana, ni wazi roho wa mauti ametanda katika anga letu.

My Country Tanzania, May God Protect thee.
 
ni mtu ambaye ubongo wake umeliwa ndio anaweza kuamini matokeo ya jana kwenye BMK, ila wenye uelewa tumeshajua ni nini.
 
Watanzania tunapaswa kuwa makini sana katika nyakati kama hizi, busara zinahitajika sana, ni wazi roho wa mauti ametanda katika anga letu.

My Country Tanzania, May God Protect thee.

BUSARA ZA WIZI LAZIMA TUWACHOME MOTO TUNAJUWA VIZURI SANA KUNZIA MJINI HADI VIJIJINI TUMESHA CHOKA HAKUNA KUTUMIA TENA BUSARA DHIDI YA WEZI KMA NYIYE HAKUNA MARIDHIANO NA MASHETANI KM NYIE HAKUNA KUPEPESA MACHO TENA NA MAFISADI KM NYIE DAWA NI KUWACHOMA MOTO TU :flame:
 
Umchome moto nani? we mjinga nini?
 
Back
Top Bottom